Bohari kuu ya dawa zanzibar imeandaa mafunzo maalum ya lugha za alama kwa wafanyakazi wake

Katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinapatikana katika sekta zote bohari kuu ya dawa zanzibar imeandaa mafunzo maalum ya lugha za alama kwa wafanyakazi wake ili viziwi wapate haki zao za msingi katika taasisi hiyo.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo katibu mkuu Wizara ya afya Bi Asha Ali Abdalla amesema wafanyakazi wanapaswa kufahamu tofauti zinazowakwaza watu wa makundi mbali mbali katika kupata huduma muhimu kama zile za afya na mawasiliano ya kawaida ili kupata jamii jumuishi.

Mkurugenzi bohari ya dawa Nd. Zahran Ali Hamad amesema mafunzo hayo yana lengo la  kupunguza matatizo yanayowakumba viziwi katika kupata muhimu ya afya na kuendeleza utumishi na utawala bora nchini.

Mwenyekiti wa chama cha viziwi CHAVITA Bi Asha Ali wameishukuru taasisi hiyo kwa kufanya mafunzo hayo na kusema ana matumaini kwa taasisi na jumuiya nyengine kufanya mafunzo hayo kwa watendaji wao ili kupunguza matatizo kwa viziwi wanapotaka huduma muhimu

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!