BARAZA LA MAASKOFU ZANZIBAR LIMEWAHIMIZA WAUMINI KUFUATA MAAGIZO YANAYOTOLEWA NA SERIKALI

Baraza la Maaskofu Zanzibar limewahimiza Waumini wa Kikristo na Wananchi kuzingatia Tahadahri na maagizo yanayotolewa na Serikali juu ya Ugonjwa wa CORONA ili kuepukana naVirusi hivyo.

Katibu  wa Baraza  hilo  Askofu Dickson Kaganga  ametowa  tamko  hilio katika  ibada  maalum  ya  maombi    ya  pamoja  kwa  Makanisa  yote   ya  kuiombea Nchi  kuepukana  na  Virusi  vya  CORONA ibada iliofanyika   katika kanisa la Kiinjli   la Kilutheri  Tanzania (KKKT) lililopo Mwanakwerekwe.

Amesema Wananchi  wote   wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima na kutekeleza maagizo yanayotolewa na Watalaam  wa Afya na kuepuka  kupokea taarifa za uongo zinazosambaa katika Mitandao ya Kijamii.

Askofu  kagaanga  amewasihi  waumini  na  Wanachi  kuishi  maisha  yanayo mpendeza  Mungu  na  kumcha  Mungu  ili  kuifanya  Dunia  kuwa  mahala  salama  pa  kuishi  na  kuwa  mbali  na  Majanga  na  Maradhi.

Baadhi ya Wachungaji walioshiriki katika Maombi hayo wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuruhusu Ibada za Jumapili na kufanya Maombi juu ya tishio la Ugonjwa wa CORONA uliyopo Duniani ili kumuomba Mwenyezi Mungu kuondoa janga hilo.

Kwa mjibu wa Takwimu  tayari Ugonjwa wa homa ya CORONA  umewakumba watu zaidi ya laki mbili na elfu 60 katika Nchi zaidi ya 160 Duniani na hadi sasa kiasi watu elfu 11 wamepoteza maisha.

Comments are closed.

error: Content is protected !!