BALOZI RAMIA AWATAKA WAKANDARASI KUMALIZA MIRADI KWA MUDA ULOPANGWA

Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa  Serikali itahakikisha inasimamia miradi ilioanzishwa ili kumalizika kwa wakati licha ya changamoto mbali mbali ikiwemo Mripuko wa Maradhi ya Corona.

Akizungumza katika Ziara ya kukagua Miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Makaazi Kwahani na Ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu Tunguu, amesema kuwepo kwa Maradhi hayo sio kikwazo cha kusimamisha Miradi ya Maendeleo na kuwataka wasimamizi waendelee na kazi zao.

Balozi amefahamisha kuwa Serikali inaendelea kufanya Tathmini ya kina ili kujua kwa kiasi gani imeathirika kiuchumia katika Sekta zake kutokana na Ugonjwa huo.

Mshauri Mwelekezi  wa Kampuni ya Arges Africa, Adrian Eradius na Mhandisi Emanuel Mushi wamesema kwa sasa Ujenzi huo Unaendelea vizuri kutokana na kuwepo vifaa vyote na wanatarajia kukamilisha Mradi huo kwa wakati waliokubaliana.

Ujenzi wa Nyumba za Makaazi za Kisasa zilizopo Kwahani umeanza Octoba 2 Mwaka jana na Unatarajiwa kumalizika Septemba Mwaka huu ambapo Ujenzi wa jengo la Mahkama Kuu Tunguu uatarajiwa kumalizika Octoba.

Comments are closed.

error: Content is protected !!