BALOZI AMINA SALUM AMEWATAKA WAFANYA BIASHARA KUFANYA KAZI NA TAASISI YA VIWANGO ZBS

Waziri wa  Biashara na Viwanda Balozi Amina  Salum amesema  ni  wajibu  kwa Wafanya  Biashara kufanya  kazi  zao  kwa  karibu  na  taasisi  ya  viwango  ZBS ili  kuinusuru  Nchi  kuwa  ghala  za  bidhaa  zisizo  na  viwango vya  ubora .

Ametoa  tamko  hilo  wakati  akifungua   Mkutano  wa  majadilioni  uliowashirikisha wafanyabiashara naZBSjuu  ya  umuhimu  wa  viwango  vya  ubora  .

Amesisittiza kuwa Wafanya  Biashara  wana  dhamana  kuwa  ya  kuwalinda  walaji  na  watumiaji wa  bidhaa  zinazozilishwa  Nchini  na  zile  zinazoagizwa kutoka  nje ya  Nchi  kwa  kuweka  mkazo zaidi  katika  matumizi ya  viwango vinavyandaliqwa kitaalamu   na  zbs kwani  vitawasaidia  kuhimili  ushindani wa Soko.

 

Mkurugenzi  wa usimamizi wa  ubora  wa  ZBS Nd. Rahima Bakari  amesema  tayari ZBS imeidhinisha  viwango  vya ubora  290 katika  bidhaa tofauti  na  kuwahimiza afanya Biashara kuvitumia  ipasavyo  ili kuwa  na  uhakika  wa  biashara  zao.

Wafanya  Biashara  wameishauri ZBS  kuiangalia  kwa  uzito unaostahiki  suala  la  kuingia  Zanzibar  kwa  bidhaa za  matunda  na  mboga  mboga zinazozalishwa  kwa  kutumia  kiwango  kikubwa cha kemikali  kwani  zina athari kubwa  kwa  watumiaji.

Comments are closed.

error: Content is protected !!