Recent Posts by Wardat Mohd

WAGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI JIMBO LA TUNGUU KWA TIKETI YA CCM WAMWAGA SERA ZAO

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wana kila sababu ya Kukithamini, Kukienzi na Kukilinda Chama chao kwa nia ya kuendelea kuwatatulia Matatizo yanayowakabili pamoja na kusimamia suala zima la Maendeleo Nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Nd.Hassan Khatib Ameeleza hayo katika Ufunguzi wa Kampeni Kibele Jimbo la Tunguu, Ambapo amewataka Wanachama hao kuipigia Kura CCM muda utakapofika kwani ina mikakati imara ya kuendeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo

Wagombea Nafasi ya Ubunge na Uwakilishi Jimbo la Tunguu wameahidi kuendlea kuboresha sekta zote muhimu, huku wakisema kuwa CCM ina nia ya kutumia fursa ya Uchumi wa buluu kwa Maendeleo ya Umma.

Mgombea Nafasi viti Maalum Uwakilishi Vijana Nd.Salha Mwinjuma amewataka Wana CCM kuendelea kuwa na imani na Chama chao na kuwaomba kuwapigia Kura Wagombea  wa CCM ili wawawakilishe Serikalini katika suala la Maendeleo ya Jimbo lao

 

CCM ZANZIBAR YAENDELEA KUNADI SERA NA ILANI KWA WANANCHI

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi Amesema katika Serikali ya Awamu ya Nane atahakikisha suala ya migogoro baina ya Wananchi na wawekezaji linapatiwa ufumbuzi.

Akizungumza katika Mkutano wa Kampeni huko Nungwi Amesema kuna baadhi ya Wawekezaji hawafuati Sheria za Uwekezaji na kusababisha Migogoro kati yao na Wananchi.

Amesema iwapo atapata Ridhaa ya kuongoza  Nchi suala hilo ataliwekea mkazo kwa kuweka mikakati madhubuti ili kuona hakuna matatizo  baina  yao na Wawekezaji kufuata sheria na utaratibu uliowekwa ndani ya Nchi.

Aidha Dk.Hussein amefahamisha kuwa atahakikisha Anawasaidia wale wote walidhulumiwa na kupatiwa haki zao za msingi

Akizungumzia kuhusu suala la unyanyasaji  wa Kijinsia kwa Watoto na Wanawake   amesema  atahakikisha anatunga Sheria ambayo itawabana Wanaofanya vitendo hivo ili visiweze kutokea kwa Wananchi

Amesema Watendaji wake wote atawasimamia ipasavyo ili kuona haki inapatikana kwa wale wote waliofanyiwa vitendo hivyo.

Akimnadi Mgombea Urais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohammed Shein Amewasisitiza Wana CCM  kuendelea kukichagua Chama kinachohubiri Amani na Utulivu pamoja na kudumisha Muungano uliyopo.

 

 

 

WANAWAKE WAJANE WAMETAKIWA KUTUMIA VIZURI MAFUNZO YA ELIMU WALIYOPATIWA

Wana Jumuiya ya Wanawake  Wajane   Zanzibar ‘Zawio’ Wameshauriwa kuitumia vyema Elimu na Mafunzo waliyopatiwa ili kulifikia lengo la kuundwa kwa Jumuiya hiyo.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh.Ayoub Muhammed Mahmoud  wakati Akizungumza na Wanajumuiya hiyo katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil  Kikwajuni  Mjini  Zanzibar.

Amesema nyenzo muhimu katika maisha ya kila Siku ni Elimu hivyo amewataka Wanajumuiya ya Wanawake Wajane kuitumia Vizuri Elimu waliyopatiwa ili kujikwamua kimaisha kama ilivyokusudiwa.
Mgeni maalum katika Mkutano huo ambae pia ni Mgombea wa Nafasi ya Uraisi wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Ali Hassan ametoa pongezi kwa Wanawake hao kujiunga katika Jumuiya hiyo na Ameahidi kushirikiana nao Pamoja na kutekeleza ahadi zote alizoziahidi kwa Jumuiya hiyo.

Kwa upande wao Wanawake wa Jumuiya hiyo Wamesema Wamefarijika sana na uwepo wa Jumuiya hiyo kwani  Wanaamini itawasaidia katika kuendesha maisha yao.

 

MH.HAJI OMAR KHERI AMEAHIDI MAKUBWA KWA WANANCHI WA TUMBATU KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI

Mgombea  Uwakilishi wa Jimbo la Tumbatu kwa Tiketi ya CCM Mh.Haji Omari Kheri amewataka Wananchi kudumisha amani na mshikamano na kuichagua CCM ili kuweza kupata Maendeleo ya katika Nchi yetu.

Ameyasema hayo  katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi zilizo jumuisha Wangombea Ubunge Udiwani na Uwakilishi huko Tumbatu  Jongowe.

Wakati huo huo Mrajis wa Chuo Kikuu cha Utawala wa Umma  (IPA ) Nd. Mshauri Abdallah Khamis amewataka   Vijana kuwa Wazalendo na kushiriki katika Shughuli mbalimbali za Kijamii ili  kuunga Mkono juhudi za Serikali za kuwalatea Maendeleo Wananchi.

Ametoa wito huo baada ya Vijana wa Vyuo Vikuu kufanya usafi klatika Hospitali ya Kivunge Mkoa Kaskazini Unguja.

Daktari dhamana wa Hospitali hiyo Dr .Amim Hamad Said Amewashukuru  Vijana hao kwa kuonyesha utu na Uzalendo.

Katibu wa Tawi la CCM Chuo cha IPA  Nd.Anuari Haji Ramadhan Ameahidi kuendelea kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Serikali.

 

Recent Comments by Wardat Mohd

No comments by Wardat Mohd yet.