Recent Posts by TALHA FERUZ

SERIKALI YA ZANZIBAR HAKUJATOA NAFASI KWA WANAMICHEZO WENGINE KUFANYA MAZOEZI YA MKUSANYIKO

Serikali  ya  Mapinduzi  ya  Zanzibar  imesema  tamko   la  kuruhusu  kuchezwa  kwa  ligi  kuu  ya  Zanzibar   hakujatoa  nafasi  kwa  Wanamichezo  wengine  kufanya  mazoezi  ya  mkusanyiko  Viwanjani  na   katika  fukwe  mbali  mbali.

Katibu  Mkuu  wa  Wizara  ya  Vijana  , Sanaa  Utamaduni  na Michezond. Omar  Hassan  kingi  ametoa  Tamko hilo  wakati akizungumza  katika  kipindi  cha  Sunday Sports cha  ZBC,  amesema   bado Wananchi  wana   wajibu  wa  kufuata  maagizo  ya Kitaalamu ya  kudhibiti  CORONA  na  kuacha  kukusanyika  katika  Viwanja  vya  Michezo.

Licha  ya  kuruhusu  kuendelea  kwa  ligi  kuu  Serikali  inaendelea  kuchukua  hatua na  Tahadhari  zote dhidi  ya  maambukizi  ya CORONA  na  kuvitaka  Vilabu  vya  Ligi kuu  ya Zanzibar  kuweka  mkazo  katika  suala  hilo  wakati  ligi  hiyo  itakapoendelea.

UADILIFU NA UMAKINI WA VIONGOZI WANAOSIMAMIA JUMUIYA ZA CHAMA ITAENDELEZA KUIMARISHA KATIBA NA ILANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  Balozi Seif Ali Iddi amesema Uadilifu na Umakini wa Viongozi wanaosimamia Jumuiya za Chama itaendeleza kuimarisha Chama hicho katika utekelezaji wa Katiba na Ilani yake.

Amesema CCM imekuwa kinapata Heshima kubwa na kuungwa mkono na Wananchi wengi  kutokana na kutekeleza kwa  Vitendo ilani na Sera zake na kuwafanya Wanachama na Viongozi wa Vyama vya Upinzani kuridhika kujiunga na Chama hicho Kikongwe Barani Afrika.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika Ofisi yake iliyomo ndani ya jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ilioongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa.

Alisema Changamoto zilizokuwa zikijichomoza ndani ya Jumuiya za chama cha Mapinduzi ambazo ziliwahushisha baadhi ya Wanachama na hata Viongozi wake kwa sasa hazistahiki kupewa Nafasi hasa ikizingatiwa kwamba Chama cha Mapinduzi katika miaka ya sasa kinaendeleshwa katika Mfumo wa Kisayansi.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwamba Taasisi hiyo imebarikiwa kuwa na Rasilmali nyingi ikilinganishwa na Jumuiya nyengine za Chama Bahati ambayo lazima waizingatie na kuisimamia ipasavyo ili lile lengo la kuanzishwa kwake lifikie pazuri.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa alisema Uongoziwa Taasisi hiyo ya Chama hivi sasa uko katika Mchakato wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika hatamu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Mheshimiwa Edmund alisema Viongozi wa Jumuiya hiyo wanaendelea na mikakati ya muda mfupi na mrefu katika kuona malengo hayo yanatimia na kuleta mafanikio waliyoyalenga.

Naye kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Visiwani Zanzibar nd. Haidar Haji Abdullah alisema suala la usafiri linapaswa kuangaliwa na kupewa msukumo mkubwa ili kuondoa changamoto inayowakabili Viongozi wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar.

 

WANAFUNZI KIDATO CHA SITA NA VYUO VIKUU, KUFANYA BIDII KATIKA MASOMO ILI KUPATA MATOKEO MAZURI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe rRziki Pembe Juma  amewataka Wanafunzi wa Kidato cha Sita na wa Vyuo Vikuu, kufanya bidii katika Masomo yao ili kupata Matokeo Mazuri katika Mitihani yao.

Akizungunza alipotembelea Skuli  zenye Wanafunzi wa Kidato cha sita  na baadhi ya Vyuo  kuangalia utaratibu wa ufundishaji wakati huu wa janga la CORONA  amesema kuwepo Maradhi hayo kusiwakatishe tamaa na kushindwa kutimiza  malengo yao katika masomo.

Mhe Riziki ameeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na  Walimu pamoja na Wanafunzi wa Vyuo na Skuli hizo katika kutekeleza masharti ya Afya ili kujikinga na Maradhi hayo.

Baadhi ya Wanafunzi hao wamezipongeza Serikali kupunguza masharti na kuvifungua Vyuo na Skuli kwavile imeleta  chachu ya kuongeza Ari ya Kusoma .

Jumla Wanafunzi Elfu mbili 687 wanatarajiwa kufanya Mitihani yao ya kidato cha sita kwa Zanzibar katika skuli 38  za binafsi na Serikali

DK. MAGUFULI AMEKUTANA NA DK. SHEIN KATIKA KIKAO CHA NDANI KILICHOFANYIKA IKULU DODOMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dkt. Ali Mohamed Shein katika Kikao cha ndani kilichofanyika ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti  wa CCM  bara nd. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally Kakurwa ambapo Viongozi hao wamezungumzia masuala ya CCM.

Baada ya kikao hicho, nd. Shein ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ameweka Udongo katika Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua Maendeleo ya Kazi ya Ujenzi wa Ofisi hizo inayofanywa na jJeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Shirika lake la Suma JKT.

Rais Shein amemshukuru Rais Magufuli amesema Kujengwa kwa Ofisi hiyo ni heshima kwa Taifa na tafsiri sahihi ya kujitawala.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwapongeza Vijana wa JKT wanaofanya kazi za Ujenzi wa Ofisi hizo,  na kuwataka kujivunia fursa hiyo ya kushiriki Maendelo ya Tanzania .

 

Recent Comments by TALHA FERUZ

No comments by TALHA FERUZ yet.

error: Content is protected !!