Recent Posts by asha farouq

WALIMU WA SKULI ZA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU MJUMUISHO

Mkuu wa wilaya ya kaskazni b Rajab Ali Rajab amewataka walimu wa skuli za mkoa wa kaskazini unguja kuyatumia vizuri mafunzo ya elimu mjumuisho ili waweze kutatuwa changamoto zinazowakabili wanafunzi katika ufahamu wao.

Wito huo ameutowa katikia skuli ya msingi mkwajuni wakati alipofunguwa mafunzo ya utambuzi wa mapema, kupima na kuwapatia huduma wanfunzi wenye changamoto za kielimu.

Amesema katika ufahamu wa wanafunzi kuna changamoto nyingi zinazowakabili ambazo walimu wanahitaji kluzifahamu mapema ili wapate urahisi wa kufundisha.

Akizitaja baadhi ya changamoto amesema kuna baadhi ya wanafunzi huwa na ufahamu mdogo na baadhi yao hadi wachukuwe muda mrefu ndio wafahamu zikiwemo sababu nyengine zinazosababishwa na malezi,makuzi,mazingira na afya.

Amefahamisha kuwa kutokana na sababu hizo ipo haja kwa walimu kuwa makini wakati wa kufundihsha na kuwatambuwa kikiamilifu wanafunzi wao ili kuhakikisaha lengo la kuwapatia elimu na kufaham7un wanchafundishwa lianafikiwa kwa mawanda mapana

Nae mwalimu Juma Salim Ali kutoka seksheni ya elimu mjumuisho na stadi za maisha zanzibar amesema wizara ya elimu na mafunzo ya amali imeamua kutoa mafunzo hayo ili walimu waweze kuwatambuwa wanafunzi wenye changamoto mbalmbali wakiwemo wenye mahitaji maaluum kwa ajili ya kuwasaidia katika masomo yao.

Amesema mafunzo hayo yatawafanya wawalimu lazima wawatambuwe wanafunzi wao katika hali tafauti na kuweza kuwasomesha kwa wanavyostahiki.

Akitowa mfano wa utambuzi amesema walimu hwataweza kuwajuwa wanafunzi viziwi,wasiona,wagonjwa wa mifupa,wenye virusi vya ukimwi,walemavu na kuweza kwenda nao vizuri wakti wanpofundisha.

Jumla ya waalimu wa skuli 6 wamepatiwa mafunzo ya stadi za maisha katika mkoa wa kazskazini unguja.

DK.ALI MOHAMED SHEIN AMEUNGANA NA WANANCHI KATIKA FUTARI MAALUM ALIYOIANDAA YEYE NA FAMILIA YAKE

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Alhaj Dk.ali mohamed shein ameungana pamoja katika futari maalum aliyoiandaa yeye na familia yake kwa ajili ya wananchi mbali mbali wakiwemo majirani zao katika makaazi yake kibele, wilaya ya kati mkoa wa kusini unguja.

Hafla hiyo ya futari ilifanyika katika viwanja vya nyumbani kwake Kibele na kuhudhuriwa na  viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, viongozi wa dini, Serikali, vyama vya siasa, wananchi wa kijiji hicho pamoja na vijiji  vya jirani.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein nae aliungana na viongozi wa kike wa Kitaifa, wanafamilia pamoja na wananchi mbali mbali wakiwemo majirani zake katika hafla hiyo ya futari maalum waliyoiandaa.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Alhaj Dk. Shein pamoja na familia yake, mwanafamilia Mohamed Ali Shein aliwashukuru waalikwa wote waliofika katika hafla hiyo na kufutari.

Katika maelezo yake, Mohamed Shein alieleza kuwa familia hiyo imefarajika sana kwa waalikwa hao kukubali mwaliko huo na kufika kwa wingi katika futari hiyo maalum waliyoiandaa.

Aidha, Alhaj Dk. Shein aliwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu wananchi wote na viongozi waliohudhuria katika futari hiyo kuendelea kupata neema na baraka za Allah hasa katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Alhaj Dk. Shein na familia yake wamekuwa na utamaduni wa kila mwaka katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuandaa futari maalum na kuwaalika wanakijiji, majirani pamoja na waalikwa wengine wakiwemo viongozi wa Serikali, dini na vyama vya siasa, futari ambayo hufanyika huko katika makaazi yake Kibele, Mkoa wa Kusini Unguja.

WANANCHI KUFUATA TARATIBU ZA UJENZI ILI KUEPUKA KUJENGA KWENYE NJIA ZA MAJI

Mkuu wa wilaya magharibi “b” captain Silima Haji amewataka  wananchi kufuata taratibu za ujenzi ili kuepuka kujenga kwenye njia za maji za asili jambo ambalo husababisha kutuama kwa maji na kuleta athari kwa wakaazi wa maeneo hayo.

Akiwa katika ziara ya kuangalia maeneo mbali mbali  yaliyoathiriwa na mvua amesema  kadri mvua zinavyoendelea kunyesha athari nyingi zimeweza kujitokeza  na kusababisha kuongezeka kwa mashimo  kwa baadhi ya maeneo  na kuleta madhara makubwa kwa wananchi hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema katika maeneo yao.

Kwa upande wao wananchi wa maeneo hayo wamewaomba wananchi wenzao kufuata taratibu zinazotolewa na viongozi hao kuhusiana na ujenzi ili kuepuka maafa hayo yanayojitokeza.

Maeneo aliyoyatembelea mkuu huyo wa wilaya  ni pamoja na kituo cha kikosi cha zimamoto mwanakwerewe pamoja fuoni mambosasa

 

MFUKO WA BIMA YA AMANA KULIPA FIDIA KWA WENYE AMANA

Spika  Baraza la wawakilish Mh; Zuberi Ali Maulid amesema bodi ya bima ya amana inajukumu la kutumia fedha za mfuko wa bima ya amana kulipa fidia kwa wenye amana, pale ambapo benki ikiwa imefungwa kwa kufilisika au kutokidhi  matakwa ya sheria.

akifungua mafunzo kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu majukumu ya bodi ya bima ya amana yaliyowashirikisha wajumbe hao.amesema ulipaji wa fidia kwa wenye amana kunaifanya jamii kuendelea kuwa na imani na mfumo mzima wa fedha hapa Tanzania.

Meneja muendeshaji kutoka bodi ya bima ya Amana nd; Rosemary Tenga, amesema lengo la kutoa mafunzo kwa wajumbe hao nikuwasaidia juu ya majukumu yao ya kazi kwa  bodi hiyo pamoja na kuisambaza elimu walioipata kwa  kuwafikia wananchi katika majimbo yao.

akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa baraza la  wawakiliashi Mh; Mohammed Ahmada mwakilishi wa jimbo la malindi ambae pia ni naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano amesema mafunzo waliyoyapata ni muhimu katika kuwawezesha katika mipango yao ya kazi pamoja na kuwasaidia wananchi juu ya kujiunga katika bima hiyo.

akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya waziri wa fedha Zanzibar naibu spika baraza la wawakilishi  Mh. Mgeni Hassan amewasisitiza wajumbe hao kuwa mabalozi kwa wananchi juu ya kufikisha ujumbe huo.

mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na bodi ya bima  ya amana kwa kushirikiana na wizara ya fedha zanzibar..

 

Recent Comments by asha farouq

No comments by asha farouq yet.