Recent Posts by asha

IDARA YA UHAMIAJI KUENDELEA KUWAJIBIKA NA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Mohammed Aboud Mohammed ameitaka idara ya uhamiaji kuendelea  kuwajibika na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuilinda zanzibar na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza katika hafla ya kuagwa wastaafu wa idara ya uhamiaji Zanzibar waliostaafu mwaka 2019 katika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul Wakil amesema kuendelea kufanya hivyo kutapunguza mianya ya wahalifu

Mhe. Aboud akitoa nasaha zake kwa wastaafu hao ameeleza kuwa katika safari ya utumishi wa umma hakuna ugumu katika maisha mapya jambo la msingi ni kumtanguliza mungu.

Kamishna wa uhamiaji zanzibar nd. Johari Sururu amewasisitiza wastaafu hao    kujumuika  vizuri na jamii pamoja na familia zao na kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii.

Akisoma risala ya wastaafu naibu kamishna mstaafu Ali Suleiman Nassor ameishukuru idara ya uhamiaji kwa mashirikiano waliyoyapata na amesisitiza kufanya kazi kwa nidhamu kwani bila ya nidhamu hakutakuwa na ufanisi katika utendaji

SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BIASHARA NA WAJASIRIAMALI

Waziri mkuu wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania mhe. Kassim Majaaliwa amesema serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya biashara na wajasiriamali ili kuweka mazingira bora zaidi ya shughuli zao.

Akifunga maonesho ya biashara ya kuadhimisha miaka 20 ya jumuiya ya Afrika mashariki majaliwa huko Fumba  amesema serikali imekua ikitoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamalina kuondosha vikwazo vya kuingizaji na kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi lengo  likiwa ni kuwapa fursa wajasiriliami kujiirimarisha katika kazi hiyo.

Waziri wa biashara na viwanda balozi Amina Salum Ali amesema na  sekta binafsi zinamchango mkubwa katika uchumi wa taifa na kutoa fursa za ajira kwa vijana na   serikali imeanzisha taasisi na mfuko maalumu kwa lengo la kutatua matatizo yanayoisu sekta hiyo.

Katika risala yao washiriki wa maenesho hayo wamewaomba wanachama wa jumiya ya Afrika mashariki kutekeleza kwa vitendo dhama ya biashara huru ndani ya jumuya hiyo na serikali kukaa na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wajasiriamali kupunguza masharti ya kupata mikopo..

 

KUTOA HABARI ZISIZO SAHIHI KUNASABABISHA VIJANA KUTOFANIKIWA MALENGO YAO

Tatizo la kutoa habari zisizo sahihi na kuiga miradi ya kibiashara kunasababisha vijana kutofanikiwa malengo yao ya kukuza uchumi na kuzikosa fursa muhimu za maendeleo.

Hayo yameelezwa na wadau katika mafunzo maalum ya kuandaa muongozo wa sera kivuli ya itakayowawezesha vijana kutumia mifuko ya uwezeshaji iliyopo nchini ambayo itawakomboa kiuchumi.

Wamesema tatizo hilo linawakatisha tamaa vijana na wengine kushindwa kujitokeza kuzitumia fursa hizo.

Waendeshaji wa mafunzo hayo wamesema wameandaa muongozo huo ambao utaisaidia serikali na pia vijana watapata uwezo wa kuitumia miradi na mifuko  itakayowainua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbali mbali za kuwaingizia kipato

WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UTALII WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI, NA MIONGOZO YA UWEKEZAJI

Wawekezaji katika sekta ya utalii wamesisitizwa kuzingatia sheria, kanuni, na miongozo ya uwekezaji kwani ndio dira ya utekelezaji wa miradi yao.

Akizungumza  katika ziara ya kuwasilisha waraka wa sheria kwa wamiliki wa hoteli mbalimbali katika mkoa wa kaskazini unguja mkurugenzi rasilimali watu wa ZIPA Vuai Yahya amesema kuwa  ziara hiyo ni agizo hilo la serekali linatokana na  baadhi ya wawekezaji wengi kwenda kinyume na makubaliano na sheria za nchi na uwekezaji.

Wawekezaji waliopokea waraka huo wameahidi kufuata sheria hizo ipasavyo, ambapo hoteli tisa zimefikishiwa waraka huo katika mkoa wa kaskazini unguja.

Ziara hiyo imejumuisha maafisa wa idara mbali mbali za serikali ikiwemo polisi, TRA, ZBR, kamisheni ya ardhi, uhamiaji, idara ya kazi na kamisheni ya utalii

Recent Comments by asha

No comments by asha yet.