AIRTEL TANZANIA YATOA BILIONI 2.5 KWA WATEJA NA MAWAKALA WANAOTOA HUDUMA YA AIRTEL MONEY

Kampuni ya simu ya mkononi ya airtel tanzania imetangaza gawio la shilingi bilioni 2.5 kwa wateja na mawakala wanaotoa huduma ya airtel money baada ya kupata kibali kutoka benki kuu ya Tanzania (BOT).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Airtel money Isack Nchumba amesema gawio hilo linawahusu wateja wa mtandao huo waliotumia huduma ya airtel money kwa kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita.

Kwa upande wake afisa habari wa kampuni hiyo jackson mbando amesema kuendana na kasi ya ukuaji wa huduma ya airtel money wamejiunga na huduma e-government ambapo wateja wake wanaweza kufanya malipo mbalimbali.

Tangu mwaka 2015 mpaka sasa kampuni hiyo imetoa kiasi cha shilingi bilioni 19 kama faida kwa wateja na mawakala wa mtandao huo Nchini

Comments are closed.

error: Content is protected !!