Wizara ya Habari  Utalii na Mambo ya Kale imesema itaendeleza Udugu na  Ushirikiano   uliopo kati ya Nchi ya Oman na  Zanzibar  kuhakikisha  wanaendeleza  Uhusiano huo licha  kufariki Mfale wa Oman Sultan Qaboos  wiki iliyopita.

Akizungumza   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Saleh  Yusuf  Mnemo   baada ya kutia saini kitabu  cha  maomlezi  pamoja  na Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo Bi Khadija Bakari huko katika Ofisi   ya   Balozi  ya Oman  Migombani   Unguja.

Wamesema wataendelea kuunga  mkono   na kuendeleza  jitihada mbali mbali za maendeleo zilizofanywa  na michango aliyoutoa kiongozi huyo wakati wa uhai wake na kumuombea   dua  Kwa   Mungu amsamehe kwani sote tutarejea kwake.

kwa upande wake balozi  Mdogo   wa Oman  Dk Ahmed Humood   Al –habs   Ameshukuru  kwa kuja kutoa mkono wa pole kwa  Viongozi wa Wizara ya Habari na kusema wapo  pamoja   katika  harakati   za kuimarisha udugu wa Damu.

Comments are closed.

error: Content is protected !!