Daily Archives: June 18, 2021

Dk. Hussein Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar kuja kuwekeza Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar  kuwaimarisha wawekezaji wa nchi hiyo ili kuja Nchini kuwekeza katika sekta za Utalii, Uvuvi pamoja na Mafuta na Gesi.

Dk. Mwinyi ametoa ombi hilo Ikulu jijini Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Hussain Ahmad Al Humaid, aliefika kujitambulisha.

Amesema tayari Zanzibar imeanzisha Sera maalum kwaajili ya kuendeleza uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wake.

Rais Dk. Mwinyi aliiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kuisaidia Zanzibar katika uimarishaji wa sekta za Maji, Afya pamoja na Elimu.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizo, na kubainisha umuhimu wa hatua hiyo kuendelezwa katika sekta binafsi.

Aidha, Dk. Mwinyi alisema kuwepo kwa safari za ndege kati ya Zanzibar na Qatar ni fursa muhimu ya kuendeleza biashara kati ya nchi mbili hizo, na kuiomba Qatar kuweka mazingira bora ya soko la bidhaa mbalimbali.

Katika hatua nyengine, Dk. Mwinyi alimshukuru balozi huyo kwa utayari wake wa kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwashajihisha wawekezaji wa nchi hiyo kuja nchini kuwekeza.

Aidha, aliiomba Serikali ya Qatar kutoa taarifa za ujio wa wanafamilia ya kifalme katika shughuli za kitalii mapema iwezekanavyo, ili waweze kupata hadhi wanazostahili.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amevitaka vyombo vya habari vifanye kazi kwa kufuata sheria.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mh Hemed Suleiman Abdulla amesema lengo la Serikali ni kuona vyombo vya habari nchini  vinafanya kazi  kwa kufuata sheria  za nchi pamoja na kufanya kazi bila ya pingamizi.

Amesema habari ikitolewa vibaya kunachangia mifarakano katika jamii.

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mh Hemed amesema hayo wakati akiahirisha mkutano wa tatu wa Baraza la kumi la wawakilishi Chukwani.

Amesema vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo ya Nchi hivyo amewaomba watendaji wa Serikali kushirikiana na waandishi  wa habari wanapotekeleza wajibu wao.

Akigusia suali la sensa  ya watu na makazi Mh Hemed ametoa wito kwa wananchi wote ifikapo muda wa zoezi la sensa  kushiriki kikamilifu na kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha zoezi hilo.

Amesema katika kuimarisha huduma za afya serikali itaendelea kuweka miundo mbinu bora ikiwemo kuanzisha bima ya afya, vifaa tiba, madawa, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na maslahi ya wafanyakazi.

Mh Hemed amesema Uchumi wa bluu unalenga kuongeza pato la Taifa kwa kutumia Rasilimali ya Bahari kwa kuwasaidia Wananchi kuinua hali zao za maisha na kuwapa uwezo waa kujiajiri na kuajiriwa.

Akimalizia hutuba yake Mh Makamu amesema Serikali ina mpango madhubuti wa kuhakikisha stahiki  za Wafanyakazi  zinapatikana kwa wakati zikiwemo posho za likizo ili kufanya kazi zao kwa ufanisi zaid.

Baraza la wawakilishi  limehairishwa hadi siku ya jumatano ya tarehe 8/September mwaka huu.

Mashekhe wa Jumuiya ya Uamsho waachiwa huru

Serikali  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania   imewaachia   huru   Mashekhe   wa   Jumuiya  ya  Uamsho  na   mihadharaya  kiislamu   Zanzibar  JUMIKI.

Taarifa  kwa  waandishi  wa  habari    iliotolewa  na   mkurugenzi  wa   mashtaka   DPP  Sylevester  Mwakitalu   imeeleza  kuwa   Serkali  imewafutia  mashtaka  yote   yaliokuwa  yakiwakabili   na  wako  huru   kuanzia tarere  17  June  2021.

Masheih    wawili   wameachiwa   kutoka  mahabusu  ambao ni Sheikh Farid hadi  Ahmed   na  Mselem  Ali  Mselem  na  wengine 34 wakisubiri  kukamilika  kwa   taratibu  za  Mahakama    ili  waachiwe   huru.

Wakizungumza   nawaandishi  wa  habari   Masheikh hao wamewaomba   waumini  wa kiislamu   kuwa  watulivu   na  wakiishukuru   Serikali   kwa    kuwafutia  mashtaka.

Mashekih   hao  walikuwa   kizuizini   takriban  miaka   tisa   wakikabiliwa    na   mashtaka   mbali  mbali   ambayo kisheria hayana  dhamana , kesi  yao  ilikuwa  ikisikiizwa  katika Mahakama  ya  Kisutu   jijini Dar es salaam.

Sheikh   Farid  hadi  na   Mselem Ali waliwasili Zanzibar  jana  na   kuungna   na   familia   zao  baada  ya   miaka  tisa.

Moto umeteketeza Kiwanda cha utengenezaji wa Samani Mwembe Njugu.

Taharuki  imewakumba   wakaazi   wa  mtaa  wa   Muembe  Njugu   baada  ya  kuzuka  kwa moto  ulioteketeza   Kiwanda   cha  utengenezaji  wa   Samani  na  kuteketeza   kiasi  kikubwa   cha   mali  na  vifaa  vilivyokuwepo    katika  eneo  hilo.

Mnamo majira ya saa nne na dakika  thalathin  asubuhi ya leo wafanyakazi wa sehemu ya kutengenezea makochi na wakaazi waliokaribu na eneo la Muembe njugu wamepata mshtuko  na  mfadhaiko  kutokan  na  moto  huo  uliodumu  kwa  takriban  saa moja  hadi ulipozimwa kuzimwa  .

Chanzo  cha  moto  huo  hadi  ZBC  inaondoka  eneo  la  tukio  kilikuwa  hakijajulika  licha ya  mmiliki  wa  Kiwanda  hicho   kudai   kushuhudia   moshi  ulliotokea   pembezni  mwa   Kiwanda   chake   na  hatimae  moto  mkubwa  ukazuka  na   kuteketeza  kila  kitu.

Moto  huo  ulidhibitiwa  kufuatia   juhudi   za   ushikiano  wa   kikosi  cha  zimamoto  na  ukokozi  kwa  kushirikiana  na   wakaazi  wa  Mwembe  Njugu   kama    inavyoelezwa  na  kamishina  wa  zimamoto   na  uokozi    kamanda  Rashind   Mzee  Abdalla.

Naibu  Mkurugenzi wa kamisheni ya kukabiliana na maafa  Muhidin Ali Muhidin akizungumza  katika eneo  la  tukio hilo   amesema  tathmini ya awali  itafanyika  ili  kujua  chanzo cha  moto  huo  na  hasara   iliojitokeza.

Hilo  ni  tukio  la pili  la  moto   kutokea  katika  Manispaa  ya   Mjini baada  ya  lile  liliotokea   katika   mtaa  wa  Kiponda mwezi  mmoja  uliopita   na  kuteketeza  nyumba  katika  eneo  la  Mji  Mkongwe hata  hivyo  hakuna  mtu  aliejeruhiwa.