Daily Archives: June 10, 2021

UWEZO WA MADAKTARI WA TANZANIA UNAWEZA KUOKOA FEDHA ZINAZOTUMIA SERIKALI KUSAFIRISHA WAGONJWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema katika kukabiliana na uhaba wa Madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, timu za madkatari wa ndani wachukue jukumu la kusaidia matibabu badala ya kutegemea kuwasafirisha nje ya nNhi.

Dk. Mwinyi amesema uwezo wa Madatari waliopo Tanzania unaridhisha hivyo kwa kushirkiana wanaweza kusaidia kumaliza tatizo hilo na kuokoa fedha nyingi inazotumia Serikali kuwapeleka Wagonjwa  wa Nje ya Nchi.

Rais wa Zanzibar amesema hayo wakati akifungua mkutano Mkuu wa 20 wa chama cha Madaktari wa upasuaji Tanzania uliofanyika Madinatul Bahar Mbweni, ambapo amesema katika  kipindi cha mwaka julai 2019 hadi sasa, Wagonjwa waliopelekwa nje ya Zanzibar kwa matibabu ni zaidi ya mia tisa na 60 na kutumia kiasi cha shilingi bilioni kumi na moja nukta saba.

Aidha Dk. Hussein Mwinyi amesema Serikali inalizingatia suala la kuimarisha maslahi ya Madaktari ili waendelee kuwahudumia wagonjwa badala ya kukimbilia katika vitengo kwa ajili ya kupata maslahi zaidi na kuasimamia upatikanaji wa vifaa tiba na Maabara.

Wakielezea matatizo yanayowakabili Madaktari wa upasuaji, Mwenyekiti wa chama cha Madaktari wa upasuaji kanda ya Zanzibar dk. Yunus Pandu Buyu amesema licha ya matatizo yaliyopo, Zanzibar imeongeza uwezo wa kufanya upasuaji wa maradhi mbalimbali kutokana na kuongeza wataalamu wakada hiyo kufikia 18 na kuishauri serikali kuandaa bajeti maalum kwa ajili ya vifaa tiba huku rais cha chama hicho Tanzania dk. Catherine Mng’ong’o ameomba kuongezwa ufadhili wa masomo kwa Madaktari wa upasuaji Nchini.

Waziri wa afya ustawi wa jamii wazee jinsia na watoto Mh. Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali inayafanyia kazi matatizo yanayowakabidhi madaktari hatua

makubwa yamefanyika kwenye sekta ya afya hasa katika Hospitali kuu ya mnazimmoja katika kutoa huduma.

Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na wataalamu zaidi ya mia moja na hamsini wa Afya kutoka Tanzania.