Monthly Archives: April 2021

SERIKALI IMEWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLIJIA

Serikali imewataka wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini kuhakikisha wanaendesha Tasnia ya Habari kwa kuendana na mabadiliko ya Teknolijia hiyo Duniani.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Ally Possi wakati akifungua kongamano la utangulizi la kuelekea siku ya Uhuru wa Habari, lililoandaliwa na Shirika la Elimu sayansi na Utamaduni la Umoja wa Taifa (UNESCO).

Amesema kwa upande wa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa Habari Nchini ili kuweza kuboresha utendaji katika tasnia hiyo ambayo inatambulika kama muhimili wa nne usio rasmi.

Pia nd. Possi amesema serikali inaheshimu na kutambua uhuru wa Vyombo vya Habari na kuwataka wanahabari kutekeza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo nchini.

Katika kongamano hili kulitolewa tunzo kwa waandishi habari Wanawake, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika tasnia hiyo na Jamii kwa ujumla

Kitaifa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari yanatarajiwa kuanza Mei Mosi na kuhitimishwa mei tatu mwaka huu ambapo kitaifa yatafanyika Mkoani Arusha.

MRADI WA AFYA

Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mh Mattar Zahor Salim amesema tafiti zimeonesha kuwa vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 wamekabiliwa na matatizo ambayo yanaathiri ustawi wa maendeleo yao kiafya na kiakili.

Mh. Zahor amesema hayo huko katika ukumbi wa Baraza la mji Chake Chake wakati akizindua mradi wa wa Elimu ya Afya ya uzazi ,hiv,na lishe kwa vijana  utakaoendeshwa na Jumuiya ya ZAPHA+ na kufadhiliwa na UNICEF.

Mh. Zahor amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya kila  juhudi katika kuwanusu vijana kuingia katika tabia hatarishi na kupoteza muelekeo wa maisha yao ya baadae.

Kwa upande wao wawezeshaji katika uzinduzi huon nd. Hassan Mahmoud Ali ambae ni Afisa stadi za maisha na ushauri nasaha kutoka Wizara ya Elimu na  mratib wa tume ya ukimu Pemba nd. Nassor Ali Abdalla wamesema mradi huo  utawasaidia vijana katika kufahamu stadi za maisha kwani umri kati ya miaka 10 hadi 19 ndio kipindi hatari kwa vijana.

Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu mashirikiano ya pamoja  yahitajika  kati ya watendaji pamoja na wadau mbali ikiwemo Wizara ya Elimu pamoja na Masheha kwani Vijana  hao wamo  ndani ya  maeneo yao.

UKATAJI WA MIKOKO OVYO NI MOJA YA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA YA BAHARINI

Ukataji wa Mikoko ovyo ni moja ya uharibifu mkubwa wa Mazingira ya Baharini yanayosababisha athari kwa Binaadamu wanaoishi karibu na maeneo hayo pamoja na Viumbe hai.

Msaidizi Mratibu wahifadhi ya Maeneo ya bahari nd. Omar Hakim Foum akizungumza wakati wa upandajimikoko katika kijiji cha Unguja Ukuu kae Pwani ikiwa ni moja ya kuadhimisha sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar amesema kumekuwa na ongezeko la ukataji wa Mikoko katika kijiji hicho ambapo imebainika kukatwa mikoko kwa kukutwa baadhi ya dhana walizokua wakizitumia ikiwemo Shoka na Mapanga.

Sheha wa Shehia ya Unguja Ukuu kae Pwani nd. Ibrahim Khamis Shomar amewataka Wananchi kuachana na tabia ya ukataji wa mikoko na badala yake wawe wasimamizi wazuri wa kuihifadhi ili iwe ni nyenzo ya fursa za ajira kwa vijana.

 

Mratibu wa Taasisi ya Jane Goodalls inayoshughulika na utunzaji wa Wanyama pamoja na mazingira nd. Ali Juma Ali ametoa wito kwa Wananchi kujitolea kutunza mali asili ya mikoko na kujiepusha na uharibifu wa maliasili hiyo ambayo inafaida kubwa kwa Taifa.

Shughuli hiyo ya upandaji wa mikoko imewajumuiya baadhi ya Wanakijiji, Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Unguja Ukuu pamoja na iongozi wa umoja wa Vijana wa CCM na Wageni kutoka nje ya Nchi.

WANAKAMATI WA MAJIMBO KUBUNI MIRADI ITAKAYOLETA TIJA NA MAENDELEO KWA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya Mjini nd.Rashid Simai Msaraka amehimizwakamati za maendeleo za majimbo kubuni miradi itakayoleta tija na maendeleo kwa wananchi kwa kuzingatia jiografia ya jimbo husika.

Akifungua mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati ya maendeleo ya Jimbo la Amani juu ya mfuko wa jimbo kupitia mwakilishimkuu huyo wa wilaya amesema mfuko unahitaji mipango imara kwa kuweka vitega uchumi ambavyo vitasaidia kukuza maendeleo ya jimbo.

Mwakilishi wa Jimbo la Amani mh Rukia Omar Ramadhan ameitaka kamati ya maendeleo kushirkiana na wananchi katika kusikiliza matatizo yanayowakabili ambayo yatasaidia kuondoka matatizo hayo ili kufikia lengo la kuwepo kwa mfuko huo wa jimbo.

Akitoa mada kwa kamati hiyo mratibu anayesimamia mfuko wa maendeleo ya jimbo wa mwakilishi kutoka ofisi ya makamo wa pili wa Rais Nassor  Khamis Mohamed amesema ni vyema kuwa makini katika matumizi ya fedha hizo ili kuepuka udanganyifu unaweza kujitokeza hali itayopelekea kutofikia lengo lililokusudiwa.

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema wameweza kufahamu namna ya mgawanyo huo wa fedha na kuahidi kuyatekeleza kwa vitendo mafunzo hayo ili kuleta maendeleo endelevu katika jimbo lao.