Daily Archives: January 19, 2021

MAREKEBISHO YA SHERIA YA JUMUIYA YA WASTAFU YA WAZEE YATASAIDIA KUPATA STAHIKI ZAO KWA MUDA MUWAFAKA

Jumuiya ya Wastaafu na Wazee wameeleza kuwa marekebisho ya Sheria ya Jumuiya hiyo yatasaidia kupata stahiki zao kwa muda muafaka.

Wakiungumza na ZBC baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa Wazee wa mapitio ya wadau wa mpangowa uwajibikaji na utekelezaji wa huduma za kinga ya jamii kwa Wazee wamesema marekebisho hayo yatawasaidia wao na wazee wajao katika kuimarisha maisha yao.

Waziri Mstaafu serikali ya Awamu ya Saba Moudiline Cyrus Castico amesema anamatumaini makubwana Raisi Dr Hussein katika kuwaenzi Wazee na kupewa stahiki zao.

Akiwasilisha taarifa juu ya mifumo ya ulinzi jamii barani Afrika nd. Salum Mohd amesema Zanzibar ni miongoni mwa Nchi Barani Afrika zenye mifumo mizuri katika suala zima la ulipaji pencheni.

SERIKALI IMEWAHIMIZA WAJASIRIAMALI KUJIPANGA NA KUINGIA KATIKA MFUMO RASMI UNAOTAMBULIKA

Serikali   imewahimiza  Wajasiriamali    kujipanga  na  kuingia  katika  Mfumo  Rasmi    unaotambulika    ili  waweze  kutambulika  na  kunufaika   na   fursa   za  kibiashara    zinazoandaliwa  na    Serikali  ili   kukuza   Biashara   zao.

Tamko  hilo  limetolewa  na  kaimu  Waziri  wa  Biashara  na  Maendeleo  ya   Viwanda   Mh  Mudrik  Soraga   wakati  akifunga  Tamasha  la  saba  la  Biashara   Maalum  kwa  Kuyaenzi   Mapinduzi  ya  Zanzibar  katika   Viwanja  vya  Maisara   na kusema   kufanya  hivyo  kutawasaidia   kupata   masoko ,  kupanua  wigo  wa   Washirika   wa Biashara  pamoja   na    Serikali  kujua  Takwimu  sahihi   na  mahoitaji  ya  Wajasiriamali  waliop  Nchini.

Katibu  Mkuu  wa  Wizara  ya  Biashara  na  Maendeleo  ya  Viwanda   nd  Juma  Reli  amesema  Serikali  inakusudia  kuanzisha   eneo  Maalum  la  kudumu   kwa  ajili  ya    Tamasha  la   biashara  kutokana   na  mafanikio  yanayopatikana    na   ongezeko  la  idadi  ya   Wafanya  biashara  wanaojittokeza  kila  mwaka .

Ufungaji  huo  wa  Tamasha  la  saba  la  Biashara  uliambatana   na utoaji  wa    vyeti  Maalum  kwa   kampuni  zilizojitokeza  kudahmini  Tamasha  hilo   na    Taasisi  zilizofanya   vizuri  katika   Tamasha  hilo lililo  washirikisha   Wafanya  biasahara    zaidi  ya  mia  tatu  .