Monthly Archives: December 2020

WATAKAOTUHUMIWA KUHUSIKA NA VITENDO VYA RUSHWA WATASIMAMISHA KAZI ILI KUPISHA UCHUNGUZI

Rais wa Z anzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Viongozi wote wa Utumishi wa Umma watakaotuhumiwa kuhusika na vitendo vya Rushwa pamoja na ukiukwaji wa Maadili, watasimamisha kazi ili kupisha Uchunguzi.

Dk. Mwinyi amesema hayo leo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa abdul-Wakili Kikwajuni Jijini hapa, wakati alipozungumza na Viongozi, watendaji na wafanyakazi wa Utumishi wa Umma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu.

Amesema mara tu baada ya kuingia Madarakani, Serikali imeanza kuwachukulia hatua za kisheria Viongozi wasiowajibika na wasioshikamana na maadili ya kazi zao, kufuatia ziara zilizofanyika katika Taasisi mbali mbali, ikiwemo bandari, Hospitali ya Mnazi Mmoja na maeneo mengine yaliomo katika mpango wa utekelezaji wa mradi wa kuendeleza huduma mjini (ZUSP).

Alisisitiza na kurejea maelezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti dhidi ya watendaji waliohusika au kutiliwa shaka ya kuhusika na vitendo vya Rushwa na ukiukwaji wa maadili; kuwa Serikali nayoiongoza itakabiliana ipasavyo na vitendo vyote vinavyoathiri utekelezaji wa misingi ya Utawala bora.

Alisema anafurahishwa na hatua ya Wananchi ya kuiunga mkono Serikali na kubainisha kuwa yeyote yule atakeatuhumiwa na hatimae kubainika hana kosa, atarejeshwa kazini na kupata haki zake kama sheria zinavyoelekeza.

“kiongozi wa umma lazima afanye kila linalowezekana kuwa mfano na kigezo cha tabia njema na ajiepushe hata na vitendo vinavyoweza kumfanya atiliwe shaka”, alisema.

Dk. Mwinyi alisema ni jambo la kusikitisha kuona taarifa iliyowasilishwa kwake kutoka zaeca , kuonyesha kuwepo tatizo kubwa la ubadhirifu wa mali za serikali na wizi katika utekelezaji wa miradi mikubwa.

Hata hivyo alisema amefurahishwa na kazi inayoendelea ya ufuatiliaji, hivyo akawataka viongozi wote watakaotuhumiwa kuhusika na ubadhirifu huo kutoa ushirikiano wa kisheria kwa chombo hicho.

“nimevutiwa sana na ari na utayari wa watendaji wa zaeca katika kufanikisha vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, tutayazingatia maombi yao waliyotueleza” , alisema.

Aidha, alisema anatambua hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali kuwa hazitowafurahisha watu wote, hivyo akawataka wananchi kuikubali hali hiyo kwa msingi kuwa wengi wataguswa, akibainisha nchi kugubikwa na muhali.

Alisema kuna miradi kadhaa mikubwa inayoonyesha kuwepo matumizi makubwa ya fedha, ambazo hazikutumika vyema (kwa mujibu wa taratibu).

Alisema wale wote watakaobainika kuhusika na uzembe, wizi au ubadhirifu wa mali ya umma, mahala popote walipo; watachukuliwa hatua  na  kusitiza azma ya seriklai katika kuzingatia haki na kuepuka maonevu.

Alipongeza kazi kubwa iliofanywa na awamu zote za serikali zilizotangulia ya kuunda taasisi na kutunga sheria zilizo bora katika kufanikisha dhana  ya uimarishaji  utawala bora, akinasibisha hatua hiyo kuwa ni ujenzi wa miundombinu iliyo bora.

Alieleza kuwa serikali imefanikiwa kuanzisha ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka, idara ya utawala bora, mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi, tume ya maadili ya viongozi wa umma pamoja na kuimarisha ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kutekeleza majukum yake kwa ufanisi.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo kuyatumia maadhimisho hayo kutafakari umuhimu wa kuendeleza maadili mema ndani ya jamii, sambamba na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia.

Aidha, aliwataka kushirikiana na jamii katika kuyakomesha vitendo hivyo pamoja na kuendeleza matumzii mazuri ya mitandao, sambamba na kupiga vita utumiaji wa dawa za kulevya.

Mapema, waziri wa nchi (or) katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora haroun ali suleiman, alitowa wito kwa wananchi  kuunga mkono juhudi za rais wa zanzibar katika kuimarisha utawala bora pamoja na kulaani kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

Aidha, aliwataka watumishi wote wa serikali kudhibiti siri za serikali na kubainisha hatua zitachukuliwa dhidi ya watumishi wasio waaminifu watakaovujisha siri hizo.

 

Viongozi mbali mbali wa kitaifa na kijamii walihudhuria mkutano huo, akiwemo makamo wa kwanza wa rais maalim seif sharif hamad, makamo wa pili wa rais hemed suleiman abdalla, katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi dk. Abdulhamid yahya mzee, jaji mkuu wa zanzibar omar othman makungu, mwanasheria mkuu wa zanzibar dk. Mwinyi talib haji, mawaziri, wakuu wa vikosi vya smz, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na wafanyakazi wa utumishi wa umma.

 

 

 

 

 

 

DK HUSSEIN ALI MWINYI AMEWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI WA TAASISI ZA SERIKALI KUPITISHA UCHUNGUZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewasimamisha kazi watendaji wa Taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kupitisha Uchunguzi kutokana na kuwepo kwa ubadhirifu wa Mali za Serikali.

Akizungumza katika  Ziara ya kutembeelea Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi ZAECA huko Victoria Gaden Dk Mwinyi amewataja watendaji waliosimamishwa kazi akiwemo  Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Bi Sabra Issa Machano, Bw Ramadhani Abdalla Ali, Kamati ya Uratibu wa Mradi wa ZUSP wa Wizara ya Fedha , Mtendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Karama Awadhi Karama pamoja na Kampuni ya Kevis Limited.

Amesema haiwezekani serikali kupoteza fedha nyingi za miradi huku baadhi ya watendaji hukwamisha juhudi hizo na kufanya ubadhilifu wa maslahi yao binafsi.

Aidha Dk Hussein ameigiza mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa Uchumi wa Nchi kufanya Uchuguzi wa mradi wa huduma za miji zanzibar ZUSP kwani  kuna viashia wa ubadhirifu wa fedha za  umma usiolingana na matumizi ya Mradhi huo.

Dk Mwinyi amepongeza Mamlaka hiyo kwa jitihada mbalimbali za utendaji wao wa kazi licha ya kuwepo kwa matatizo yanayowakabili katika kutekeleza Majukumu yao kazi.

Akisoma taarifa fupi Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi ZAECA Bw. Mussa aji ali amesemamamalaka hiyo katika kipindi cha mwaka jana wamefanikiwa kuokoa zaidi ya shillingi Millioni mia mbili ambazo hadi sasa wanaendelea kufanya Uchunguzi kwa baadhi ya miradi ikiwemo Ujenzi wa Barabara Kaskazini a na  ole kengeja kwa Pemba.

MAJINA NANE YA WAJUMBE WA KAMATI YA UHAMASISHAJI WAKATI WA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI CUP

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Omar Hassan Kingi ametangaza Majina Nane ya Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji wakati wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup.

Kamati hiyo itakayojumuisha Wajumbe kutoka Zanzibar na Tanzania Bara itaongozwa na Mwenyekiti Taufiq Salim Tturkey ambae ni mbunge wa Jimbo la Mpendae na Wajumbe wengine saba ambao ni Hassan Mussa Ibrahim (Has T), Salum Issa Ameir, Mwanahawa Rajab Iddi, Khamis Mwinjuma (Mwana Fa) Jeri Muro,  Salama Jabir na Ali Saleh (Albato).

Akitangaza Majina hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Tabia Maulid Mwita amesema lengo la Kamati hiyo ni kunogesha  na kuwahamasisha Wananchi kupitia Wasanii wa Sanaa za Asili, Maigizo na kizazi  kipya ili kuwezesha kufana kwa Sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha amesema Kamati hiyo itakuwa na Majukumu ya kuratibu na kusimamia Wasanii pamoja na upatikanaji wa Fedha kutoka kwa Wadau wa michezo, Wafadhili na Taasisi Binafsi kwa ajili ya uendeshaji wa Michuano hiyo.

Kingi pia ameitumia fursa hiyo kuwashajihisha Wananchi kushiriki kwa wingi katika Michuano hiyo yenye mnasaba wa kuyaenzi   Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Hamasa za Wasanii mbali mbali zitatumbuizwa kabla ya  Mechi, wakati wa mapumziko na baada ya Mechi.

 

CHANGAMOTO ZA MUUNGANO KUONDOLEWA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepongeza juhudi za makusudi zinazoendelea kuchukuliwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuondoa changamoto za Muungano.

Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar katika mazungumzo kati yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Mwalimu aliyefika Ikulu kwa ajili ya Kujitambulisha.

Rais Dk. Hussein Mwinyi alipongeza hatua hiyo ambayo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa makusudi katika kutatua changamoto hizo na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo italeta mafanikio makubwa kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa mategemeo yake ni kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto hizo na kueleza kwamba kwa yake yanayohusu ngazi za juu kwa upande wao wako tayari kuyafanyia kazi ili kufikia pale palipokusudiwa.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Maziringira Mhe. Ummy Mwalimu alitumia fursa hiyo kwa kuanza kumpongeza Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi na wananchi wa Zanzibar.

Waziri Mwalimu ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Muungano Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alieleza matumaini yake kwamba Zanzibar itafika mbali na kupata mafanikio makubwa kutokana na uongozi wa Rais Dk. Mwinyi hasa kutokana na kasi yake ya kutaka kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Ummy Mwalimu alimueleza Rais Dk. Hussein mwinyi juhudi za makusudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kuzipatia ufumbuzi changamoto za Muungano ambazo kwa kiasi kikubwa juhudi hizo zimezaa matunda.

Aliongeza kwamba nyingi ya changamoto hizo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi na zilizobaki ambazo ni chache utakeleza wake unatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika vikao vitavyokaa kati yaviongozi wa SMT na SMZ.

Sambamba na hayo, Waziri Ummy Mwalimu alieleza azma ya kukaa kikao cha Kamati  ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa kuondoa changamoto zilizobaki.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Mohammed Salum alisema kuwa mbali ya Waziri Mwalimu kuja kujitambulisha kwa Rais pia, Waziri huyo anatarajia kufanya ziara katika miradi ya Maendeleo ya Jamii (TASAF) pamoja na miradi ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijini(MIVAP).

Miongoni mwa mafanikio katika kutatua changamoto zilizopo mnamo Oktoba 17 mwaka huu 2020, SMT na SMZ zilisaini hati za makubaliano ya kuondoa hoja tano za changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ambapo nyengine sita zinasubiri kupatiwa ridhaa ya kikao cha Kamati ya Pamoja kati ya SMT na SMZ ili nazo ziondolewe kabisa.

Kuondolewa kwa hoja hizoni miongoni mwa utaratibu wa kawaida wa kurekebisha changamoto zilizopo sambamba na kuuendeleza, kuuenzi, kuulinda na kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao tayari umeshatimia miaka 56 tokea kuasisiwa kwake.