Daily Archives: November 3, 2020

DK. HUSSEIN MWINYI AMEWAPONGEZA WAZANZIBARI KUJITOKEZA KUTUMIA HAKI YAO YA KIKATIBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza Wazanzibari kote Nchini kwa kujitokeza kwa wingi na kutumia vyema haki yao ya kikatiba ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Dk. Mwinyi ametowa pongezi hizo leo katika sherehe za kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduziya Zanzibar, hafla liyofanyika katika Uwanjawa Amani Jijiji hapa.

Amesema hatua ya wananchi haokujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na hatimae kukichaguwa Chama cha Mapinduzi ni kielelezo cha kukomaa kisisasa na kidemokrasia, kwa kutambua kuwa uchaguzi uliohuru na haki ndio njia sahihi ya kupata viongozi wataongoza Serikali kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dk. Mwinyi alisema Serikali atakayoiunda itaongozwa kwa misingi ya haki, uwajibikaji, uwazi n ausawa kwa wananchi wote bila kumbagua mtu kutokana na itikadi yake, jinsia au eneoa nalotoka.

Aliwashukuru Mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali yakimataifa walioshiriki katika sherehe hizo na kubainisha kuwepo kwao kunathibitisha uhusiano mwema uliopo katiya Zanzibar na nchi zao.

Mapema, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibuwa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdul hamid Yahya Mzee alimkaribisha Rais wa Zanzibar ,akibainisha hamu waliyo nayo wnanachi ya kumsikiliza.

Sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya nanae ya Serikali ya Mapinduziya Zanzibar, ziliambatanana Kiapo gwaride la Vikosi vyaUlinzi naUsalama, Onyesho la Ndege zaKivita,kikosi maalum cha Kamondoo wa JWTZ