Daily Archives: October 30, 2020

MATOKEO YA URAIS ZANZIBAR

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ametangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Zanzibar baada ya kuwashinda Wagombea wenzake 16 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Dk. Hussein Mwinyi amepata Kura laki Tatu, Elfu Thamanini, Mia nne na Mbili kati ya kura laki nne, elfu thamanini na saba, mia nane na 42.

akimtangaza mshindi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud amesema Dk.Hussein Mwinyi ameshinda kwa asilimia 76 nukta 27.

Matokeo hayo yanafuatia kukamilika kwa matokeo ya Urais kwa Majimbo yote 50 na kuonyesha kuwa Dk. Mwinyi amsehinda.

Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad anashikilia nafasi ya Pili kwa kupata asilimia 19 ya kura.

Jumla ya Wagombea 17 wa vyama mbali mbali vya siasa walishiriki katika Uchaguzi wa Rais uliofanyika jana.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kimeongoza kwa kupata uwakilishi mkubwa katika Baraza la Wawakilishi ambapo imeshinda viti 45 kati ya Hamsini huku ikipata idadi kama hiyo kwa upande wa Ubunge na kupata viti vingi vya Udiwani.

chama cha ACT Wazalendo kimepata viti vinne vya uwakilishi na chama cha wananchi CUF kimepata kiti kimoja.

 

WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA WATOA SHUKURANI BAADA YA MATOKEO YA URAIS

Rais Mteule wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amewahimiza Wazanzibari kuendelea kuwa kitu kimoja katika kujenga Zanzibar mpya.

Akizungumza baada ya kutangazwa Mshindi wa Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu huko Maruhubi, Dk. mwinyi ameahidi kuendeleza mema na kujenga Imani kwa Wananchi.

Amesema baada ya Uchaguzi kumalizika Jukumu kubwa lililobakia ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa kitu kimoja kufanya kazi za Maendeleo.

Dk. Mwinyi aliyechaguliwa kuongoza Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema anakishukuru chama cha Mapinduzi na Wanachama wake kwa kuamini kumpa ridhaa na kuahidi kutowaangusha.

Wakati huo huoakizungumza kwa niaba ya Wagombea wenzake Mgombea wa Ada Tadea nd. Juma Ali Khatibu amewashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa kufanya Uchaguzi wa Kistarabu na wao kwa ujumla wamekubaliana na Matokeo ya Uchaguzi na kuwataka Wapinzani wote kumuunga Mkono Rais Mteule Dk. Hussein Mwinyi kufanya kazi za kuleta Maendeleo.