Daily Archives: October 21, 2020

WAZEE WA KIJIJI CHA BWELEO KUZIDISHA UMOJA NA MASHIRIKIANO ILI KUENDELEZA MAENDELEO KIJIJINI HAPO

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi amewasisitiza Wazee wa Kijiji cha Bweleo kuzidisha umoja na Mashirikiano ndio njia muhimu ya kuendeleza maendeleo Kijijini hapo ambapo yatawafanya vijana wa Kijiji hicho kuweza kuyaendeleza.

Akizungumza na Wazee wakati wa kulizinduwa Baraza hilo la Wazee amesema kuwepo kwa Baraza la Wazee katika Vijiji unasaidia kuondosha migogoro katika Jamii.

Amesema ni vyema kwa vijana kujifunza historia ya Vijiji vyao ambayo kwa sasa vijana wengi wanashindwa kuzijuwa Historia ya Vijiji vyao pamoja na Nchi yao.

Wakisoma Risala kwa niaba ya Wazee hao ndugu Ali Makame Mataka amesema Kijiji cha Bweleo kina kumbukumbu za miaka mingi katika utaratibu wa Uongozi wa Baraza la Wazee na kuweza kufanikiwa katika malengo mingi ya kijamii hivyo kufunguzi wa Baraza hilo litaleta tija kwa Jamii.

Mzee Ali Mwinyijuma Kirobo amesema hapo mwanzo lilikuwepo Baraza ya ili kwa sasa linatakiwa kufanya kazi zaidi kwa maslahi ya Kijiji hicho.

 

WAFANYAKAZI WA WIZARA YA FEDHA WAMETAKIWA KUWA WAAMINIFU ILI KUIWEZESHA SERIKALI KUPATA MAPATO

Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdi wawa amewataka Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha kufanyakazi kwa nidhamu na uaminifu pamoja na kujiepusha na tamaa ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa ajili ya mipango yake ya Maendeleo.

Akizungumza katika Mkutano wa kuwaaga Wafanyakazi wa Wizara  hiyo Mh: Ramia  amesema  Wizara ya Fedha imekuwa na  vishawishi vingi vinavyohusiana na masuala ya Fedha  vinavyopelekea kutokuwa waaminifu hivyo amewasisitiza  Wafanyakazi hao   kuwa waadilifu   na kukinai kwa kile wanachokipata.

Aidha ameziomba Taasisi za kifedha kamavile Mabenki ,TRA, ZRB na Bima kuwa makini katika kufuatilia madeni  ya Serikali  ili Fedha hizo ziweze kupatikana  kwa matumizi ya Serikali.

Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khatibu Muhiddin Khatibu amesema  katika kipindi chote  cha Uongozi wa Mh. Ramia wameshuhudia  umahiri  busara na  miongozo yake ambayo yamewezesha kufanyakazi zao kwa ufanisi bora .

Kwa upande wake Afisa Mdhamini izara ya Fedha na mipango  Ibrahim Saleh Juma kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara hiyo  wamemshukuru Mh: Ramia kwa mashirikiano yake na Wafanyakazi  ambayo yamewapa hamasa  pamoja na kuwajengea misingi imara ya kiutendaji.

Mapema Mh:Ramia ametembelea na kukagua jengo la Ofisi za Serikali  zilioko Gombani  Chake Chake  ili kuona mafanikio na Changamoto za Wafanyakazi.