Daily Archives: October 13, 2020

SERIKALI INAENDELEZA UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA ZA GHOROFA KATIKA MAENEO MBALI MBALI NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Sheni amesema Serikali itahakikisha inaendeleza Ujenzi wa Nyumba za kisasa za ghorofa katika maeneo mbali mbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na Wananchi katika Uzinduzi wa Nyumba Mpya za kisasa huko Kwahani amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali ijayo itaendeleza Ujenzi wa Nyumba za maendeleo ikiwa ni wazo la Muasisi wa Mapinduzi Shekh Abeid Aman Karume ili kupunguza matumizi ya Ardhi.

Akieleza  kuhusu Ujenzi wa Nyumba hizo Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abidiwawa amesema   makaazi hayo Mapya ya Wananchi wa Kwahani ni hatua moja wapo ya kuleta mabadiliko kwa Wananchi sambamba na kuwa na makaazi bora na ya kisasa.

Nae Mgombea Rais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa  Mbunge wa Jimbo la Kwahani amesema  Serikali ya Awamu ya Saba imetekeleza miradi mingi kivitendo endapo  watamchagua atahakikisha yale mazuri yote  yaliyofanywa anayaendeleza.

Katika Risala yao Wananchi wa Kwahani wamemshukuru Dk Shein kwa mengi mazuri aliyoyafanya na kumtakia mapumziko mema.

Ujenzi huo wa Nyumba za Ghorofa Kwahani kwa Awamu ya kwanza umegharimu shilingi Bilioni 10.6 nukta sita.