Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr. John Joseph Pombe Magufuli amesema bado Muungano una manufaa makubwa kwa pande zote mbili na ni kipaumbele cha kwanza cha serikali ijayo baada ya Uchaguzi
Akiwahutubia mamia ya wana CCM na Wananchi katika mkutano wake wa kwanza wa kampeni hapa zanzibar dr magufuli amba e pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Amefahamisha kuwa katika kipindi cha takribani Miaka Arobain ya Muungano huo Zanzibar imefaidika na utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye gharama ya takriban zaidi ya Shillingi Trillion mbili nukta tatu Fedha zilizoenda moja kwa moja kwa SMZ.
Amekanusha kuwa sio kweli kwamba Zanzibar imekuwa hainufaiki na mapato ya muungano huo na kuwahakikishia wananchi wa zanzibar kuwa hata pale itakapoanza kuchimba Mafuta na Gesi asilia mapato yatakayotokana na Rasilimali hizo yatabaki kuwa ya Zanzibar na sio vyenginevyo.
Dr Magufuli amewaomba wananchi wa Zanzibar kumchagua Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Zanzbar ili aweze kushirikiana nae kuleta mabadiliko makubwa ya Maendeleo hasa katika sekta ya uwekezaji , Elimu , Uchumi wa Bahari kuu , Miundo mbinu na Kilimo.
Mgombea wa Urais wa zanzibar kupitia CCM Dr Hussein Ali Mwinyi nae ameahidi kuulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwa na mipango bora ya kuinua uchumi wa Zanzibar ili uweze kuwanufaisha watu wote na kuleta tija kwa Taifa.