Daily Archives: September 17, 2020

DK. MWINYI AMEAHIDI ONGEZEKO LA UCHUMI ZANZIBAR

Mgombea  wa  Urais  wa  Zanzibar  kwa  Tiketi  ya  Chama  cha  Mapinduzi  CCM Dr.Hussein Ali Mwinyi   Amesema  dhamira  ya  Serikali  ijayo  ya kuwa  na  Uchumi  mpya  inaweza  kutimia  iwapo  Wazanzibar  wataamua  kufanya  kazi  kwa  bidii  .

Akizungumza  na  Mamia  ya  Wana chama  wa  Chama  hicho  katika  Uwanja  wa  Gombani  ya kale Kisiwani Pemba  amefahamisha  kuwa   uwajibikaji  ndio  kipaumbele  cha  kwanza  katika  Serikali  atakayoiongoza hivyo,  kila  mmoja  kwa  nafasi  yake  ni lazima  ahakikishe anatimiza  Wajibu  wake .

Akizungumzia  masuala  ya  Kiuchumi   Dr.Hussein  amesema mkazo  zaidi  utawekwa  katika  kuimarisha  Sekta  ya  Utalii  kwa  kuwa  na  Utalii  utakaowanufaisha  Wananchi  katika  nyanja  zote  pamoja  na  kupandisha  kiwango  cha  Elimu.

Dr.Mwinyi amesema  Serikali  ya  Awamu  ya  Nane  itasimama  imara  kupambana  na  vitendo  vya Udhalilishaji  kwa  kuhakikisha   Viongozi  wa  Serikali  katika  Maeneo  yao  wanawajibika  kudhibiti  Vitendo  hivyo.

Naye Rais  wa  Zanzibar  na  Mwenyekiti  wa  Baraza  la  Mapinduzi  Dr.Ali  Mohamed  Shein  amewahimiza  Wananchi  Kisiwani  Pemba  kumuamini   Dr.Hussen Mwinyi na  kumpa  kura  kwani  ana uwezo wa kuiongoza  Zanzibar  na  kuleta  Maendeleo  Makubwa.

 

MAAFISA RASILIMALI WATU WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI

Mafisa Rasilimali Watu kutoka Taasisi mbali mbali Wamesisitizwa kuzingatia Wajibu wao ili kufanya kazi zao kwa ufanisi ikiwemo Utunzaji wa Kumbukumbu za Wafanyakazi kwa Usahihi.

Akifungua Semina ya Maafisa hao iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, Kamishna wa Idara ya Kazi Nd.Fatma Iddi Ali Amesema hatua hiyo itajenga upeo katika utendaji na kuondosha usumbufu kwa watendaji Wanapostaafu kazi.

Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Nd. Ali Suleiman Ahmad Amesema Mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa katika kukumbushana na kubadilisha Taarifa juu ya uwekaji wa Kumbukumbu za Mafao.

Akiwasilisha mada kuhusu Usajili Nd.Rajab Haji Machano Amesema Baadhi ya Maafisa Rasilimali Watu wanashindwa kukamilisha  Vielelezo vinavyotakiwa wakati wa usajili jambo linalopelekea usumbufu kwa Wastaafu.

Washiriki Wasemina hiyo wametoa shukran kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa kuwapatia Mafunzo hayo.

error: Content is protected !!