Daily Archives: September 15, 2020

TCRA IMETOA MAFUNZO KWA WADAU WA MAWASILIANO NCHINI JUU YA USALAMA WA MATUMIZI YA MITANDAO

Serikali kupitia   Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Tcra   imejipanga katika swala zima la utoaji wa Mafunzo   kwa Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa njia za Mitandao zinakuwa salama kupitia Matumizi ya Teknolojia mbalimbali

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Ofisi ya Tcra Zanzibar Nd.Esuvatie Aisa Masinga wakati Akifungua Mafunzo ya Usalama wa Mifumo ya Tehama Zanzibar kwa Maafisa Tehama kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali Amesema   ni vyema Maafisa hao wakawa na uwezo zaidi wa Utunzaji wa   siri za Taasisi kwa kupambana Matukio ya kiusalama katika Mifumo ya Tehama   na kulinda   kudhibiti mifumo hiyo katika Taasisi wanazozifanyia kazi

Washiriki wa Mafunzo hayo wameimba Serikali kupitia Mamala ya Tcra kutoa Mafunzo hayo mara kwa mara kwa lengo la kukabiliana na Wahalifu wanaotumia Mitandao kwa kuhujumu mali pamoja na uvujaji wa siri za Tasisi za Serikali kutokana na kukuwa kwa Teknolojia

Mkufunzi kutoka   Tcra Amesema Mafunzo wanayoyatoa ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maafisa hao katika Utendaji wa kazi zao sambamba na utunzaji na udhibiti wa Data katika Mitando

Mafunzo hayo ya Siku tano yametolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Tcra kwa kushirikiana na Serkali kwa lengo la kupambana na Wahalifu wa Mitandaoni

 

 

 

WANANCHI WAMEISHUKURU SERIKALI KUTOKANA NA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA BARABARA YA MWERA MAMBOSASA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh.Haji Omar Kheri Amesema kukamilika kwa Ujenzi wa Barabara ya Mwera Mambosasa  kutaendeleza  kuchangia  pato la Nchi.

Akizungumza katika Ukaguzi wa Barabara hiyo Mh.Kheri Amesema Barabara hiyo itasaidia kuimarisha shughuli za Biashara kwa Wananchi na kupelekea kuongeza pato la Nchi.

Aidha amewaomba Madereva wa Gari za Mizigo kutopitisha Gari zao yenye zaidi ya Tani kumi ili kudumu kwa muda Mrefu kwa Vizazi vya  sasa na baadae.

Wakaazi wa Eneo hilo Wamesifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo Ujenzi wa Barabara hiyo na kusema kuwa itarahisisha Shughuli za Usafirishaji hasa Biashara ambapo itasaidia kuongeza Pato lao na Taifa.

Barabara hiyo ya Mwera Mambosasa ina Urefu wa Kilometa 3 Nukta 5 inajengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Kukamilika kwa Ujenzi wa Barabara hiyo yenye Urefu wa Kilometa 3.5 utachochea Shughuli za Kiuchumi na kutarahisisha Shughuli za Kimaendeleo Nchini.

 

error: Content is protected !!