Daily Archives: September 11, 2020

DK.MWINYI AMETOA SHUKRANI KWA WANANCHI WA JIMBO LA KWAHANI

Wanachama  wa  Chama  cha  Mapinduzi  wana  kila  Wajibu  wa  kuhakikisha   Amani  na  utlivu  wa  Nchi  unaimarika   wakati  wa  Kampeni  na  Uchaguzi  kwani  ndio  nyenzo  muhimu  kwa  Nchi  ya  Kidemokrasia.

Tamko  hilo limetolewa  na   Mgombea wa   Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi  Dr.Hussein  Mwinyi   wakati wa Kikao maalum na Wananchi  wa Jimbo la Kwahani cha kutoa shukrani  kwa Kumchagua kuwa Mbunge wao kwa  Awamu 3 na kuwasisitiza  kuzigatia  suala  la  Amani.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama  Ndugu Talib Ali Talib kutanguliza  mbele  uzalendo  na  kufanya  kazi  pamoja  katika  kufanikisha  ushindi  wa  CCM ili  kiendelee  kushika  Dola.

Wakaazi  wa Kwahani wameelezea Hisia zao juu ya Maamuzi sahihi ya CCM ya Kumchagua Dr. Hussein kupeperusha Bendera ya Chama hicho  kwa Nafasi ya Urais wa Zanzibar na kuahidi  Kumuunga  Mkono   pamoja  na  kumpatia  Zawadi  Mgombea  huyo.

WANANCHI WA KIJIJI CHA NUNGWI WAMETAKIWA KUILINDA MIUNDOMBINU WANAYOWEKEWA NA SERIKALI

Wametakiwa kutumia Vyema Miundombinu inayoanzishwa na Serekali au Taasisi Binafsi  kwa lengo la Kujikwamua na Umasikini.

Akikagua maendeleo ya Soko linalojengwa na kufanyiwa Ukarabati kwa baadhi ya Sehemu huko Nungwi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Nd. Omar Ali Amir amewataka Wavuvi kuacha kutumia Vibanda vilivyojengwa kiholela Nje ya Soko hilo ambavyo vinaharibu haiba na Mandhari ya hapo.

Amesema iwapo watalitumia vizuri Soko hilo litaweza kupandisha thamani ya bidhaa zao  na kupata tija  kiuchumi.

Mkurugenzi wa Idara maendeleo ya Uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema Serikali imeamua kuyapatia Ufumbuzi matatizo ya Wavuvi katika Maeneo yao ili kuendesha Harakati zao  na Mazingira bora ya kuuzia Samaki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uvuvi ya Nungwi kwa Niaba ya Wavuvi Wenzake     Nd.Kibabe Adibu Amesema Soko hilo wameomba kujengewa Uzio  ili liwe katika Mazingira salama.

Soko hilo la Nungwi linafanyiwa Ukarabati na Kujengwa kwa baadhi ya Maeneo chini ya ufadhili wa Mradi wa usimamizi wa Ukanda wa Bahari ya Kusini mwa Bahari ya Hindi na limegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 150 kwa  usimamizi wa Serikali Kuu.

 

 

VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUTOTOSHEKA NA ELIMU WALIYOKUWA NAYO

Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar inawataka Vijana wa Karakana za Magari kutotosheka na Elimu waliyokuwa nayo kwenye Taaluma ya Ufundi ili waendane  na mabadiliko ya kasi ya Teknolojia ya Sayansi Duniani.

Akifungua Warsha ya Siku Moja ya Majadiliano ya Fursa na mahitaji ya kiufundi katika Fani ya Ufundi Magari kwa Zanzibar katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzoo ya Amali Dr.Bakari Ali Silima Amewataka Mafundi hao kuwa na Muamko wa ufanisi wa utendaji unaoendana na Mahitaji ya Serikali.

Amesema Mamlaka ya Amali inashirikiana na Sekta Binafsi kwa kuwanyanyua Walimu na Mafundi wa Magari  kwa kuwapatia Mbinu za Kufundisha pamoja na kuwapatia vifaa  vitakavyokidhi mahitaji na kukuza uwelewa katika kazi zao.

Akitoa ufafanuzi kwa Washiriki hao Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Nd.Hamad Hamad amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuimarisha Vyuo vya Amali kwa kuunda Mitaala mipya  na kuibua Vipaji vipya vinavyoendana na wakati uliopo kwenye Karakana zote za  Magari.

Washiriki wa Warsha hiyo wamezishukuru Taasisi hizo kwa kuwapatia Fursa za kuengeza Elimu  ambayo itawasaidia  Kuajiriwa au kujiajiri wenyewe  na kuongeza pato la Nchi.

Warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa Ushirikiano na Jumuiya ya Wafanya Biashara na Viwanda na Serikali ya Ujerumani .

 

error: Content is protected !!