Daily Archives: September 10, 2020

NACTE KUPATIA UFUMBUZI TATIZO LA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUPATA NAMBA YA TUZO YA UHAKIKI KWA WAKATI 2 views•Sep 10, 2020

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma amelitaka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE kanda ya Zanzibar  kulipatia ufumbuzi tatizo la Wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu la kupata namba ya Tunzo ya uhakiki avn kwa wakati.

Akizungumza katika Ofisi za NACTE Kanda ya Zanzibar Kinazini Mhe. Riziki amesema amepokea malalamiko kutoka kwa Wanafunzi juu ya usumbufu wa kupata avn,hali inayowakatisha tamaa ya kujiunga na vyuo Vikuu kwa mwaka huu.

 Afisa mdhamini wa nacte kanda ya Zanzibar Bw. Mohammed Abdallah Mbasha amesema NACTE inafanya kazi  kwa karibu na Vyuo Vikuu vya Zanzibar kuhakikisha Wanafunzi wanaingia katika mfumo kwa wakati, lakini mara nyingi Vyuo vyenyewe vinachelewesha kuingiza matokeo ya Wanafunzi wao.

Wakati huo huo Mhe Riziki amefanya Ziara Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ya Tanzania kanda ya Zanzibar kinazini na kuwataka kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria zinazohusu kulipa Mikopo hiyo.

Maafisa wa Bodi hiyo wamewaomba Maafisa Utumishi wa Taasisi na Wizara mbalimbali za binafsi na Serikali kuorodhesha  majina ya wanaowajiri mapema  ili kuepusha usumbufu wa kurejesha Mikopo.

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!