Daily Archives: September 9, 2020

MAMA SAMIA AMWAGA SERA ZA CCM KIGAMBONI

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema katika kipindi cha Miaka Mitano kijacho yaani 2020-2025 kimepanga kununua Meli Tano za Uvuvi, kujenga Bandari ya Uvuvi katika Ukanda wa Pwani pamoja na kumalizia Miradi yote ya Maendeleo ambayo bado haijakamilika na kuanzisha mingene ili kuweza kuchochea maendeleo kwa watanzania.

 Kauli hiyo imetolewa na Mgombe Mweza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mama Samia Suluhu Hassani mbele ya Maelfu ya Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es saalam, waliojitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni katika Wilaya hiyo.

Amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi imejipanga kikamilifu kutekeleza Miradi ya Maendeleo iliyopo na kuanzia mipya ikiweomo Ujenzi wa Barabara za Juu katika Jiji la Dar es salaam, Miradi ya Maji, Umeme, Barabara Bwawa la kuzalisha Umeme pamoja na Reli ya Kisasa.

Aidha Mama Samia amesema Serikali ya CCM itaendelea kusisitiza uwekezaji katika Viwanda Nchi ili kuweza kupunguza tatizo la Ajira na kuagiza Bidhaa kutoka Nje ya Nchi.

Awali amkimkarisha Mgombea Mweza, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Nd.Kate Kamba amewaomba Wanaccm na Watanzania kwa Ujumla kutofanya makosa kwa kuwachagua Wagombea wa upinzani huku akisisitiza kuwa Viongozi  bora  wanatoka  ndani ya CCM.

Nae Mgombe Ubunge Jimbo la Kigamboni Dkt Faustini Ndungurile wameomba wana Kigamboni na Watanzania kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi katika Miaka Mitano mingine ili kiweze kutekeleza Miradi mbalimbali na kulinda Amani na utulivu  uliopo  Nchini.

Katika Mkutano huo Mama Samia Suluhu Hassani alimuombe Kura Mgombe Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli, na  Mbunge na Madiwani wa Jimbo la Kigamboni pamoja na kumpokea Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Chadema  Kadawa Lucas Limbo Aliyeamua Kujiunga  na CCM.

 

BALOZI SEIF AMEIPONGEZA KAMPUNI YA BASRA TEXTILE MILLES KWA KUKIFUFUA KIWANDA CHA NGUO CHA COTEX

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Kampuni ya Uwekezaji ya Basra Textile Milles kwa kazi kubwa ya kukifufua upya Kiwanda cha nguo cha Cotex kilichopo Mtaa wa Chumbuni inayokweda sambamba na azma ya Serikali ya kuimaisha Sekta ya Viwanda Nchini.

Akifanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya uimarishaji wa miundombinu ya Kiwanda hicho inayotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu kwa Awamu ya kwanza Balozi Seif alisema hiyo ni kazi nzuri ambayo faida itakayopatikana itasaidia  sio kwa wawekezaji bali kwa Taifa na Vijana katika suala la ajira.

Alisema kiwanda cha Cotex kwa miaka mingi kimekuwa eneo la magofu lililokuwa likilalamikiwa na Wananchi kwa kutoendelezwa licha ya Serikali Kuu Kiwanda hicho kumpa Muwekezaji aliyeshindwa kukiendeleza kwa Zaidi ya Miaka 25 iliyopita nyuma.

Balozi Seif alisema nia thabiti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwashawishi Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi kuanzisha miradi ya Kiuchumi itakayosaidia kutoa ajira kwa kundi kubwa la Vijana sambamba na kuongeza Mapato ya Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuendelea kutoa msukumo ili kuona malengo ya kuanzishwa Mradi huo kwa vile yanawagusa Wananchi moja kwa moja yaweze kufanikiwa.

Mapema akimtembeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho hicho Bwana Ahmed Osman Osman Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda alisema harakati zinazoendelea hivi sasa ni ufungwaji wa mashine ili kukamilisha Awamu ya Kwanza.

Bwana Osman alisema majaribio ya kwanza wa uzalishaji wa Kiwanda hicho unatarajiwa kuanza rasmi Mwezi Oktoba mwaka huu kwa hatua za uzalishaji wa Vitenge, Vitambaa vya sare za Skuli, Mashuka ya Vitanda vya Majumbani na hata Mahotelini.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Basra Textile Milles Bwana Said Hassan alimueleza Balozi Seif kwamba Awamu ya kwanza iliyochukuwa gharama za Dola za Kimarekani Milioni 21.3 itawezesha kutoa ajira 454 za Wafanyakazina  Awamu ya Pili Wafanyakazi 1,200.

Bwana Said Hassan alisema Awamu ya Tatu itakayotoa ajira 1,600 itakwenda sambamba na ununuzi wa zao la Pamba kutoka Tanzania bara ili kuimarisha uwezo wa Wakulima Wazalendo.Alifahamisha kwamba yapomatumaini makubwa ya ubora wa mashine zilizopo kuzalisha bidhaa za kiwango cha juu kwa asilimia 90% kitakachosafirishwa katika masoko ya Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.

Akitoa shukrani katika ziara hiyo Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Mohamed Ramia aliuhakikishia Uongozi wa Kiwanda hicho kwamba Serikali kupitia Wizara hiyo inazingatia kuzipatia ufumbuzi changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza wakati wa harakati za uimarishaji wa Kiwanda hicho.

Balozi Ramia alisema Kiwandi hicho kilichoanza kuwa tegemeo kubwa la ajira kwa kundi la Vijana ni eneo muhimu litaloleta faida kwa Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar.

 

 

 

 

 

WAVUVI WA KIJIJI CHA CHWAKA WAILILIA SERIKALI JUU YA VIFAA VYA KUTENDEA KAZI

Upatikanaji wa Vifaa vya Kisasa vya Uvuvi  vitasaidia kufikia Uvuvi wa Bahari Kuu wenye tija zaidi katika kuwakomboa Wananchi Kiuchumi .

Wakilalamikia  kuwepo kwa Vifaa visivyokidhi haja Wavuvi wa Chwaka wamesema  iwapo watapatiwa Nyenzo za Kisasa wataweza Kuvua Maji makubwa  na Kuwaacha Samaki Wadogo waweze kukua ili kuongeza Mapambano ya Uvuvi Haramu.

Wamesema ukilinganisha na hali ya sasa Kiuchumi imekuwa Vigumu kutokana na wingi wa Wavuvi  wakizingatia uchache wa Vyombo kunaleta  msongamano katika harakati za Uvuvi katika kujikimu kimaisha.

Aidha wameiomba Serikali kuwapunguzia Gharama za ukataji Leseni za Uvuvi hasa  katika kipindi hichi kigumu kutokana na hali ya Upepo kunachangia ukosefu wa Samaki Baharini .

 

error: Content is protected !!