Daily Archives: September 8, 2020

SERIKALI HAIRIDHISHWI NA HATUA YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA KUU LILIOPO TUNGUU

Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Ramia Mohamed Abdiwawa amesema Serikali hairidhishwi na hatua ya Ujenzi wa jengo jipya la Mahakama kuu liliopo Tunguu .

Kauli hiyo ameitoa  baada ya kukagua hatua ya Ujenzi ya jengo hilo ambapo Balozi Ramia amesema kutoridhika na Ujenzi huo kunatokana na muda uliobaki ni mdogo   na bado kuna maeneo mengi hayajakamilika.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi hiyo ya maendeleo hivyo ni Jukumu la wasimamizi kuhakikisha jengo hilo linakuwa imara na lenye ubora unaotakiwa.

Amesema kumekuwa na visingizio vinavyotolewa na baadhi ya Wakandarasi katika Miradi mingi ya Serikali ikiwemo kukosekana kwa rasilimali ya mchanga hivyo amebainisha kuwa visingizio hivyo visiwe sababu ya kuchelewa kwa mradi huo.

 

error: Content is protected !!