Daily Archives: September 7, 2020

BALOZI SEIF AMEWATAKA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUENDELEZA UMOJA NA AMANI NDANI YA CHAMA

Wagombea wa Nafasi mbalimbali za Uongozi  kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi wametakiwa kuendeleza Umoja na  Ushirikiano   baina yao  ili kukipatia Ushindi na Mafanikio Chama hicho.

Akizungumza na Wagombea wa Nafasi za Ubunge  Uwakilishi na Udiwani katika Ukumbi wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Kichama  Mgombea Nafasi ya Uraisi kupitia Chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi  amesema  ni vizuri kwa Wagombea hao kuwa  Wamoja  na kuondoa tofauti zao katika Kipindi cha Kampeni ili kufikia Malengo ya Chama cha Mapinduzi

Aidha Amesema Chama cha Mapinduzi kimefanya Maamuzi ya kufanya Mikutano ya Ndani kwa lengo la kufikisha zaidi Sera za Chama kwa Wananchi na kuweza kuziunga Mkono na ameahidi kufanya kazi kwa Uwezo wake wote kwa ajili ya kutetea Maslahi ya Wananchi wa Zanzibari.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa  ya Chama cha Mapinduzi Mh.Balozi Seif Ali Iddi Amesema Chama cha Mapinduzi kimejipanga vyema katika kudumisha Amani na Utulivu wa Nchi  katika kipindi chote cha Kampeni na Uchaguzi Mkuu.

Aidha amewataka Viongozi wote watakaoshinda katika Uchaguzi Kufanya kazi kwa ukaribu na Wananchi ili kuzidisha Ushirikiano Pamoja na kutatua Changamoto zinazowakabili Wananchi hao kwa Wepesi.

DK. HUSSEIN MWINYI AMEWATAKA VIJANA NCHINI KUTHAMINI MICHEZO KWA KUWEZA KUJIAJIRI KUPITIA SEKTA HIO

Vijana Wametakiwa kuthamini Michezo kwani imekuwa ni Ajira ya Kudumu ambayo inaweza kubadilisha Maisha kwa kuwaingizia Kipato.

Akizungumza katika Mashindano ya Yamle Yamle katika Uwanja wa Magirisi Meli Nne Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi amesema Vijana wanawezo Mkubwa wa kujiajiri kupitia Sekta ya Michezo ambayo imekuwa ikiimarika Duniani kote.

Nae Mratibu wa Mashindano hayo Nd.Jecha Simai Jecha Amesema wapo katika hatua za Mwisho kumaliza Makundi huku Akipongeza ujio wa Dk.Mwinyi katika Mashindano hayo ambapo Mchezo wa Leo  Timu ya Taifa Tangini Kutoka Bwejuu wamefanikiwa kuifunga Timu ya Anfiled ya Bububu Bao 1-0 .

WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA BOTI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUZAMA

Watu Watatu Wamefariki Dunia baada ya Boti waliokuwa  Wakisafiria kuzama wakati Wakielekea Dar es salaam Wakitokea Bandarini Kizimkazi.

Akithibitisha tukio hilo Afisa wa Kikosi cha KMKM Kambi  ya  Kizimkazi P/O Abdallah Amour  Amewataja Waliofariki kuwa ni Nd.Khadija Mohammed Bakar, Aisha Said na Tatu Makamba

Amesema Abiria Mmoja hajapatikana hadi sasa  na  ametambulika kwa Jina la Francis Cosmas.

Ameeleza kuwa Boti iliopata Ajali hiyo ilipakia Abiria 15  ambapo Wengine Wameokolewa na Kikosi hicho kwa kushirikiana na Raia Wema.

Daktari wa Hospitali ya Makunduchi Amour Muhsin Burhan Amesema Watu hao Wamefariki baada ya Kunywa maji mengi  ya  Bahari na kusababisha Vifo hivyo

 

 

WASANII WA TASNIA YA FILAMU NCHINI WAMETAKIWA KUJIONGEZA KITAALUMA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo   Nd.Amour Hamil Bakar Amewasisitiza Wasanii wa Tasnia ya Filamu Zanzibar kujiongeza Kitaaluma ili wapate fursa za kujifunza zaidi nafasi inapotokezea.

Akifunga Mafunzo ya Siku Kumi ya kuwajengea uwezo Wasanii Waandaaji wa Filamu pamoja na Waandishi wa Filamu Zanzibar Naibu Katibu Mkuu huyo Amesema Zanzibar ina Fursa ya kuwa na Wasanii wenye Uwezo wa kuzalisha Filamu zenye Viwango, ila kinacho wakwamisha ni uhaba wa Taaluma ya Tasnia hiyo.

Msimamizi na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Cosoza Zanzibar Ndugu Mtumwa Khatib Ameir, Amesema endapo Wasanii hao  wataitumia Taaluma walioipata katika Mafunzo hayo ya Siku 10 itawasaidia kukuza kipato cha Wasanii hao.

Wakufunzi wa Mafunzo hayo wamesema kazi za Wasanii hao zinaweza kuwa za Kimataifa iwapo Watapata Mafunzo ya ziada katika masuala ya Taa, Uungaji Picha na Sauti.

Washiriki wa Mafunzo hayo wameipongeza Taasisi ya Cosoza pamoja Wakufunzi wa Mafunzo hayo na kusema kuwa ni imani yao kuwa Mafunzo waliopatiwa, yamewaongezea Ujuzi zaidi na ni Matumaini yao kuwa Watafanya kazi zenye Ubora wa hali ya juu.

 

 

error: Content is protected !!