Daily Archives: September 5, 2020

DK. HUSSEIN MWINYI AMEKUTANA NA WAZEE WA CCM WA MKOA WA KUSINI UNGUJA

Mgombea wa Urais  wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Husein Ali Hassan Mwinyi amewataka Wazee wa Mkoa wa Kusini  kuwacha makundi nakudumisha Umoja na mshikamano  ili  Mkoa huo uendelee kuwa Ngome ya CCM.

Dk. Mwinyi ameeleza hayo alipokukutana na Wazee na Wanaccm wa Mkoa huo na kuzungumzia masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu

Amesema Mkoa wa Kusini Unguja unatambulika Tanzania nzima kuwa ndio Ngome kuu ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi hivyo Umoja na Mshikaamano ndio msingi pekee utakaopelekea kupatikana kwa Ushindi katika Uchaguzi Mkuu

Aidha amesisitiza kudumisha Amani na Utulivu uliopo Nchini ili kuendeleza maendeleo  yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Saba katika nyanja mbali mbali za  Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh.Ayoub Mohamed Mahmod  amefahamisha kuwa kitendo cha kuzungumza na Wazee wa Mkoa huo kimewapa faraja Wazee hao na kumpa Baraka katika Safari ya kuelekea Uchaguzi Mkuu

Wazee wa Mkoa huo wamemuhakikishia Dk. Hussein Mwinyi kwamba watakua Mstari wa mbele  na watajitokeza kwa wingi wakati wa Kupigia  Kura ili Chama cha Mapinduzi  kuweze kushinda kwa Kishindo

IGP SIRO AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI PAMOJA VYAMA VYA SIASA KUEDELEA KUHIMIZA AMANI YA NCHI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP  Saimon Siro Amewataka  Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi  wa Dini Kisiwani Pemba kuendelea kuwahamasisha Wafuasi wao umuhimu wa Amani na Utulivu Nchini  kabla na Baada ya Uchaguzi.

IGP Siro  Ameyasema hayo huko  katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi  wakati alipokuwa  Akizungumza  na Viongozi  wa Vyama  vya Siasa na Viongozi  wa Dini katika  kuelekea Uchaguzi Mkuu.

IGP Siro Amesema kila Mmoja anawajibu wa  kutekeleza Sheria bila shuruti  wakati wote  hivyo  ni vyema kwa Viongozi hao  kufuata  sheria na taratibu  ili kuona kila Mmoja anatekeleza matakwa yake  kwa Amani na Utulivu .

Nae Kamishna wa Jeshi la Polisi  Zanzibar   Mohammed Haji   Hassan Amewataka  Viongozi hao kushirikiana  kwa nguvu zote  katika kuhakikisha  Amani inaendelea  kuwepo.

Mapema Akizungumza  katika  hafla  hiyo  Mkuu wa Mkoa  Kusini Pemba Mh.Hemed Suleiman Abdalla  amewaasa  Viongozi  wa Vyama vya Siasa pamoja na Wanachi  kutokuvunja Sheria  kwa kuchukua  hatua  Mikononi mwao na badala yake  kufuata  Sheria.

Wakichangia  katika Mkutano huo baadhi ya Viongozi hao   wamewataka Viongozi Wenzao pamoja na Wananchi  kuweza kuzuia  Nafsi  zao  kwa kumtanguliza Mungu mbele  ili kuona  Jamii inabaki Salama.

 

 

MH. MAHMOUD THABIT KOMBO AMESAIN KITABU CHA MAOMBELEZO KUFUATI KIFO CHA RAIS WA ZAMANI WA INDIA

Serikali ya  Mapinduzi ya  Zanzibar imesema itaendeleza Ushirikiano wa  Kidugu na  Muda  Mrefu  uliopo   baina  ya Zanzibar na Serikali ya India ili  kuimarisha Uhusiano uliopo kati  ya  Nchi  hizo .

Akizungumza  baada ya Utiaji Saini wa Kitabu cha Maombolezo   kufuatia   Kifo cha  Raisi Wazamani wa India  Pranab Mukherjeekatika Afisi  za   Ubalozi Mdogo wa India Migombani  kilichotokea hivi karibuni Nchini India Waziri wa habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo amesema  Serikali  na  Wanachi  wa  Zanzibar  wameshtushwa   na  Kifo  hicho  na  kuwaomba   Wananchi  wa  India  kuwa  Wastahamilivu .

Amemuelezea  Rais  huyo  wa  Zamani  wa  India  kuwa  ni  Kiongozi  alieipenda  Nchi  yake na  kuiongoza  Kizalendo  na  kuwa  na  Mchango  Mkubwa  kwa  Maendeleo   ya  Taifa  hilo  lenye  idadi  kubwa  ya  Watu  Barani  Asia.

Mh  .Mahmoud  Amesisitiza  kuwa   India  na  Zanzibar   ni  Washirika  wa  muda  Mrefu  na  kwamba  Nchi  hizo  zitaendelea   kushirikiana  katika  Nyanja  mbalimbali    za  Kimaendeleo  ikiwemo  Afya  , Elimu  , Miundombinu   na   Fursa  za  Mafunzo   .

Kaimu Mkurugenzi wa  Idara   ya Mambo ya Nje  Kombo Abdulhamid  Khamis  Amesema Uhusiano  wa  Tanzania  na  India  umekuwa  na  manufaa  makubwa  kwa  pande  zote  Mbili  hivyo  kuna  kila  sababu  ya  kuimarishwa  katika  nyanja  zote.

Balozi Mdogo wa India aliepo  Zanzibar  Mh.Bhahwant  Singh  ameishukuru Serikali ya Zanzibar kwa kuwa nao bega kwa bega  Wakati  huu  wa  Msiba  huo  Mzito na kuahidi kuendeleza ushirikiano  uliopo kati ya Serikali zote Mbili.

Rais wa  Pranab  Mukherjee   Alikuwa  ni  Rais  wa Kumi  na  Tatu  wa  Taifa  h

error: Content is protected !!