Daily Archives: September 4, 2020

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR WAMETAKIWA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KWA UFASAHA

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Bi Mahfudha Alely amewahimiza Wafanyakazi wa Shirika lake kufanyakazi kwa ufanisi na kutumia Lugha ya Kiswahili kwa ufasaha wake.

Akizungumza katika Mkutano na Wafanyakazi wa ZBC amesema Wafanyakazi wakiwajibika vizuri shirika litaendelea kuwa bora na kuongeza imani kwa Wananchi kwa kupata Habari na Taaluma mbali mbali.

Amesisitiza Wafanyakazi hao kuongeza nidhamu ambayo ndio inayoleta tija katika utendaji wa kila siku na hayopo tayari kuona au kusikia watendaji wanakosa nidhamu na maadili ya kazi zao.

Akizungumzia mpango wa Shirika kupunguzwa  kwa Wafanyakazi Mjumbe wa Bodi Nd. Ali Bakar amesema mpango huo unakusudia kuwahamisha baadhi ya Wafanyakazi na sio kuwafukuza kazi na unalengo la kuliboresha Shirika hilo.

Akizungumzia maslahi ya Wafanyakazi Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Nd. Chande Omar amesema Shirika linaendelea kuangalia kwa karibu maslahi bora kwa watendaji wake hasa kwa kuzingatia ugumu wa kazi zao.

Nao wafanyakazi wa vitengo tofauti hawakuwa nyuma kuzungumzia vikwazo katika utendaji wao.

Mkutano huo ni wa kwanza kati ya wafanyakazi wa shirika la utangazaji na bodi yao.

 

error: Content is protected !!