Daily Archives: September 3, 2020

DR. HUSSEIN MWINYI AREJESHA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

Mgombea nafasi ya Urais  kupitia  Chama cha Mapinduzi  CCM  Dk. Hussein Mwinyi amekuwa Mgombea wa kwanza kurejesha fomu katika Tume ya Uchaguzi baada ya kukamilisha taratibu.

Mwenyekiti waTume ya Uchaguzi Jaji Mstahafu Hamid Mahamoud akipokea fomu hizo amesema  Tume imeridhika  na namna ya ilivyojazwa Fomu.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Mhe. Hussein Mwinyi amesema atatoa kipaombele Elimu na kuzidi kuimarisha miundombinu.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Nd.Abdalla Juma Sadala, Mabodi, amekutana na Waandishi wa Habari hapo katika Ukumbi wa Afisi Kuu CCM Kisiwandui ambapo Amesema Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na Baadhi ya kauli zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa zinazoashiria uvunjifu wa Amani utulivu na Usalama uliopo Nchini.

Aidha amefahamisha kuwa Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuilinda Amani tulionayo huku akiwataka Wagombea Nafasi za Uongozi kutoa ahadi zinazotekelezeka wakati wa kampeni utakapowadia.

MH. HASSAN AMEWASHUKURU WANANCHI WA SHEHIA ZA HAWAI KWA KUKUBALI KUPISHA UJENZI WA BARABARA

Mkuu  wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Hassan Khatib Hassan amewashukuru wananchi wa shehia za Hawaii na Michikichini kwa kukubali kuondosha sehemu ya nyumba zao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara.

Mhe Hassan ametoa shukrani hizo huko Shehia ya Hawaii wilaya ya Magharibi A katika Mkutano maalumu na Wananchi wa Shehia mbili hizo kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara itakayopita katika maeneo yao.

Amesema kitendo cha Wananchi hao kukubali kuvunja sehemu ya makaazi yao yaliozidi kwa hiari kutapelekea kutimiza azma ya Serikali katika kuimarisha Miundombinu na kuwazogezea karibu huduma za kijamii Wananchi wake.

“Kwa dhati ya moyo wangu na kwa niaba ya serikali nikushukuruni wananchi wa shehia ya Hawaii na Michikichini kwa kitendo chenu cha kuridhia kuondoa sehemu ya Majengo yenu kwa ajili ya ujenzi wa Barabara”alisema Mhe Hassan.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameutaka uongozi wa Shehia ya Hawaii kuundaa mipango ya Ujenzi wa Hospitali katika eneo hilo ili kupunguza masafa  kwa Wananchi wa Eneo hilo kufuata Huduma ya aAfya katika Maeneo ya jirani.

“Sheha najua hapa lipo eneo linalotarajiwa kujengwa skuli ni eneo kubwa katika eneo lilelile shirikianeni na manispaa kuandaa michoro ambayo litakuwepo jengo la hospitali utakapomalika Ujenzi wa Barabara basi Skuli na Hospitali nazo zijengwe”alisema Mkuu wa Mkoa.

Nao Wananchi wa Shehia hizo mbili wamemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa ya kuwajengea Barabara katika Shehia zao.

Hata hivyo Wananchi hao wameuomba Uongozi wa Serikali ya Mkoa kuwaondolea baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi na salama,umeme kuwa mdogo na kuwekea matuta wakati itakapokamilika Ujenzi wa Barabara hiyo.

Barabara hiyo ya Hawaii mchikichini yenye urefu wa kilomita mbili na upana wa mita saba ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

error: Content is protected !!