Daily Archives: September 2, 2020

UMAKINI ULIYOFANYWA NA WAJUMBE WA BODI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI UMELETA MANUFAA MAKUBWA

Waziri wa Habari Utalii na mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesifu kazi nzuri ya Umakini iliyofanywa na Wajumbe wa bodi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ambyo imeleta manufaa makubwa.

Akivunja na kuwaaga Wajumbe wa Bodi hiyo kutokana na Chuo hicho kuunganishwa na Chuo Kikuu cha Taifa SUZA amesema Manufaa hayo yamepelekea kuinyanyua zaidi Tasnia ya habari na kuwaomba kuendelea kutoa Michango yao kwa ,Maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Bi Aiman  Duwe amesema Bodi hiyo imefanya Kazi zake kwa kuzingatia zaidi Uzalendo na weledi mkubwa jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kukiletea Maendeleo Chuo hicho.

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi hiyo Bw. Hamad Bakar Mshindo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuthamini mchango wa Bodi hiyo na kuahidi kuendeleza mazuri kwa kutoa michango yao pindi watakapohitajika.

 

error: Content is protected !!