Daily Archives: September 1, 2020

WAASTAAFU WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR WAMETAKIWA KUTOA UJUZI WAO KWA WAFANYAKAZI WENGINE

Shirika la Utangazaji Zanzibar limewataka Wastaafu wa Shirika hilo kushirikiana katika kutoa Ujuzi wao kwa Wafanyakazi wengine ili kuhakikisha linaendelea kutimiza malengo yake ya kutoa Taarifa za uhakika kwa Jamii.

Akizungumza na Wastaafu wa Shirika la Utangazaji Naibu Mkurugenzi Bi Nassra Mohamed amesema kuondoka kwa Wafanyakazi hao sio mwisho wa kushirikiana kwa kutoa ujuzi wao hivyo ni vyema kuwa pamoja na Wafanyakazi wengine hasa wanaoingia katika ajira ili shirika liendelee kufanyakazi zake kwa ufanisi.

Wastaafu hao wakiwemo Mtangazaji wa Redio Bi Hasina  Suleiman  na Omari Khamis wameushukuru Uongozi Shirika hilo na kuahidi kutoa ushirikiano wao pamoja na kuutaka Uongozi wa Shirika hilo kuepukana na Ubaguzi katika Kazi.

 

error: Content is protected !!