Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetiliana saini na Kampuni ya Salim Construcrion na Kampuni ya Badri East Afrika, makabidhiano ya majengo ya maabara za Kisayansi Kumi na Mojaya Unguja.
Akizungumza baada ya Utiaji huo wa saini uliofanyika Mazizini,katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Muhandisi Idrisa Muslim Hija amesema kukamilika kwa Maabara hizo ni hatua ya kuendelea kukuza Sekta ya Elimu hasa katika Masomo ya Sayansi.
Aidha amefahamisha kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaendelea kuboresha Elimu Nchini kwa kuimarisha Miundo mbinu Taaluma za Walimu wa Masomo mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Mipango Sera na utafiti wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali bwana Khalid Masoud Waziri amesema Wizara yake imeridhishwa na Ujenzi wa Majengo ya Maabara hizo.
Mshauri elekezi wa mradi wa ZISP msanifu majengo bwana Ntobangi amewataka Wakandarasi wa majengo hayo kupokea matengenezo yatakayojitokeza kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Wakandarasi wa Majengo hayo wameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa ushirikiano waliounesha wakati wote wa Ujenzi wa Maabara hizo.