Daily Archives: August 30, 2020

DKT MAGUFULI AMEAHIDI KUJENGA UWANJA MKUBWA WA KISASA WA MICHEZO DODOMA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa kisasa wa Michezo utakaokwenda sambamba na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.

Akizungumza katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma amesema hatua hiyo na nyenginezo zinalenga kuimarisha zaidi Jiji la Dodoma.

Dkt Magufuli amesema Watanzania wanataka mabadiliko katika Sekta mbali mbali jambo ambalo linatekelezwa katika hatua tofati.

Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kulinda Rasilimali za Madini, kupambana na Rushwa Ununuzi wa Ndege Mpya 11 na kurejesha nidhamu kwa watendaji wa Umma.

Aidha ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa Ndege Mjini Dodoma utakaokuwa na uwezo wa kusafirisha Abiria moja kwa moja kuelekea Nchi za Nje.

Sambamba na hayo amesema Serikali itanunua Ndege nyengine mpya Tano ikiwemo ya kubebea Mizigo.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ali akitoa muhutasari wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 amesema inalenga kuhimiza Wananchi kuwa Wazalendo kwa Nchi yao na kutunza Rasilimali za Taifa ziwe chachu ya Maendeleo.

Amesema ataendelea kuilinda Amani na Mapinduzi ya Zanzibar ili kuimarisha maendeleo ya Tanzania.

MAKABIDHIANO YA MAJENGO YA MAABARA ZA KISAYANSI KUMI NA MOJA YA UNGUJA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetiliana saini na Kampuni ya Salim Construcrion na Kampuni ya Badri East Afrika, makabidhiano ya majengo ya maabara za Kisayansi Kumi na Mojaya Unguja.

Akizungumza baada ya Utiaji huo wa saini uliofanyika Mazizini,katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Muhandisi Idrisa Muslim Hija amesema kukamilika kwa Maabara hizo ni hatua ya kuendelea  kukuza Sekta ya Elimu hasa katika Masomo ya Sayansi.

Aidha amefahamisha kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaendelea kuboresha Elimu Nchini kwa kuimarisha Miundo mbinu Taaluma za Walimu wa Masomo mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Mipango Sera na utafiti wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali bwana Khalid Masoud Waziri amesema Wizara yake imeridhishwa na Ujenzi wa Majengo ya Maabara hizo.

Mshauri elekezi wa mradi wa ZISP msanifu majengo bwana Ntobangi amewataka Wakandarasi wa majengo hayo kupokea matengenezo yatakayojitokeza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wakandarasi wa Majengo hayo wameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa ushirikiano waliounesha wakati wote wa Ujenzi wa Maabara hizo.

 

TIMU YA AUTO BRAZIL IMETOKA SARE YA BAO 1-1 DHIDI YA BANGALOO FC YA MAKUNDUCHI

Timu ya  Auto Brazil wamedhidi jiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika hatua ya 32 bora baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Bangaloo FC ya Makunduchi katika michuano ya Yamle Yamle yanayoendelea ndani ya Dimba la Magirisi arena .

Auto Brazil waliovalia Jezi rangi ya Manjano wamekubali kutoka sare katika Mchezo huo ambao uliokuwa wa kuvutia katika muda wote wa Mchezo.

Makocha wa Timu hizo wamesema Michuano hiyo imezidi kuwa mingumu hasa katika kuielekea ya 32 bora.

Wakati Mashabiki wanaofika Kiwanjani hapo wamejigamba kwa Timu zo kuzidi kufanya vizuri katika Michuano hiyo.

 

error: Content is protected !!