Daily Archives: August 28, 2020

DK.SHEIN AMEONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM ,Kisiwandui Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine Kikao hicho kimepokea na kujadili Taarifa ya mapendekezo ya Wana CCM walioomba kuteuliwa Kugombea Nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, kutoka katika Majimbo na Nafasi ya Uwakilishi Viti Maalum vya Wanawake katika Mikoa ya Zanzibar.

Kikao hicho ni Maalum kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 1977.

Aidha Chama cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni Miongoni mwa Vikao vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya CCM.

 

 

MABINGWA WATETEZI WA MASHINDANO YA YAMLE YAMLE CUP WAONESHA MAKUCHA YAO

Mabingwa Watetezi wa Mashindano ya Yamle Yamle Timu ya Uzi City kutoka Meli Nne Uzi wamefufua matumaini ya kutetea taji lao baada ya Jioni ya leo kuwafunga Timu ya urafiki kutoka Donge Mabao 3-0, katika Uwanja wa Meli Nne Magirisi.

Uzi City waliyovalia Jezi rangi ya chungwa walianza kwa kishindo katika mchezo huo na kuwachukua mpaka dk 20 kuanza kupata bao la kwanza lililofungwa na Yussuf Juma dakika 20 na 30 ambapo bao la tatu likifungwa na Khelef Mido dakika 77.

ZBC Michezo ikazungumza na Mashabiki waliyofika kushuhudia Mashindano hayo huku wakiipongeza ZBC  na kuomba kuendelewa kila Mwaka Mashindano hayo.

WAUMINI WA DINI MBALI MBALI VISIWANI UNGUJA WAKUSANYIKA KUIOMBEA NCHI AMANI KATIKA UCHAGUZI UJAO

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu na Kikristo kuendelea kuiombea Nchi Amani hasa katika kipindi hichi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza katika Kongamano la Amani ambalo limefanyika katika Viwanja vya Maisara, Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa msimamizi wa Amani ni Mwanachi Mwenyewe hivyo kila Mtu anawajibika kuisimamia ili isije ikatoweka.

Viongozi wa Dini wamesema ni vyema kuwepo na mienendo mizuri ya kuepuka vichocheo vitakavyosababisha machafuko.

Mchungaji Edward Lenjima kutoka Kanisa la Pentekoste akisoma Risala ameelezea lengo kuu la Kongamano hilo ni kuomba Amani, kuuombea Uchaguzi uwe wa salama pamoja na kuombea Uchumi wa Nchi.

 

JAMII YA WAHINDI WANAOISHI ZANZIBAR WAHITIMISHA IBADA YA ISHVAR YA SIKU TANO

Jamii ya Dini ya Hindu Zanzibar wamehitimisha ibaada Ishvar ya Siku Tano ambayo kila Mwaka hufanyika Duniani kote.

wakiadhimisha siku hiyo kucheza na maandamano yaliyoanzia Kiponda mpaka Shangani ambayo kwao ni Siku ya raha na kupata Baraka Waumini wa Dini hiyo wamesema kila Mwaka hukusanyika kwa kuwa Siku hiyo kwao huondolewa Mikosi , Nuksi  na kuwachwa na Baraka kwao.

Aidha Wamesema  Mungu wao ambae anatambulika kwa Jina la Ishvar anaondoka na kumtupa Pwani huku akiwa amewaachia Baraka na Aman na Upendo.

error: Content is protected !!