Daily Archives: August 27, 2020

ZEC IMEMKABIDHI FOMU YA KUWANIA NAFASI YA URAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINY

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imemkabidhi fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi ambae anaegombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi

Dk Hussein Mwinyi  amechukua fomu hizo saa tatu asubuhi katika  ofisi ya ZEC maisara na kusindikizwa na wanachama wa CCM.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu Dk Mwinyi amesema moja ya kipaumbele chake ni kukuza Uchumi na kuwapatia vijana Ajira

Aidha amevutaka vyama vya siasa kushindana kwa hoja ili wafanye kampeni za amani katika Uchaguzi ujao

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar Mh. Hamid Mahamoud amesema amemkabidhi fomu hizo baada ya mgombea kukidhi vigezo na masharti ya Uchaguzi.

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!