Daily Archives: August 26, 2020

BALOZI SEIF AMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUILINDA MIUNDO MBINU YA BARABARA ZAO

Wakati Serikali Kuu ikiendeleza dhima ya kuimarisha Miundombinu ya Mawasiliano ya Bara Bara Nchini kwa kutumia gharama kubwa Wananchi wana wajibu wa kuzingatia matumizi bora ya rasilmali hiyo muhimu katika mwenendo wa Uchumi wa Taifa pamoja na ustawi wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati alipofanya Ziara mahsusi ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Bara Bara Nne zinazojengwa katika kiwango cha lami chini ya usimamizi wa Mfuko wa Bara bara Zanzibar pamoja na Benki ya Kiarabu inayosimamia Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika {Badea}.

Bara bara hizo ni pamoja na ile iliyoanzia Kinduni hadi Kitope yenye Urefu wa kilomita nne, Mwera Mambo Sasa hadi Mashine ya Maji Meli Tano ikiwa na urefu wa kilomita 3.4, Fuoni Polisi hadi Kibonde Mzungu Daraja la Dr. Shein kilomita 1.2 pamoja na  ile  iliyoanzia Mtaa wa Jumbi hadi Koani kilomita 6.3.

Balozi Seif  alielezea kuridhika kwake na kazi kubwa inayofanywa na Wahandisi Wazalendo katika kuweka Miundombinu safi na imara ya Bara bara jambo ambalo litaleta faraja kubwa kwake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein wakati wa Mapumziko yao baada ya Utumishi wa Umma.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashauri Wahandisi hao wakati wanapokabidhiwa jukumu la kuimarisha Miundombinu ya Ujenzi wakazingatia vyema mbinu na mikakati ya kisasa katika Ujenzi huo kutokana na uhaba wa Rasilmali ya Mchanga unaovikabili Visiwa vya Zanzibar hivi sasa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishauri Wizara inayosimamia masuala ya Ujenzi pamoja na ile ya Fedha kuhakikisha kwamba suala la malipo linafanyika kabla ya kukabidhiwa Miradi husika kwani haitopendeleza kuona Mradi unamalizika na kukabidhiwa ukiwa bado unakabiliwa na Deni.

Balozi Seif alitoa onyo kwa  Vijana wanaoendesha Vyombo vya Moto kwa Mwendo wa Kasi kuacha mara moja tabia hiyo mbaya na isiyostahiki kwa Mila na Utamaduni wa Asili kwa vile  unagharimu maisha ya Wananchitu kadhaa hususan Wazee na Watoto wasio na hatia yoyote.

Wakitoa ufafanuzi wa kazi zinazoendelea za Ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Bara bara Wahandisi wasimamizi wa miradi hiyo walisema yapo matumaini makubwa ya miradi hiyo ya bara bara kukamilika katika kipindi kilichowekwa kwa mujibu wa mikataba yake.

Walisema hatua hiyo imekuja kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoupata wa Wananchi katika sehemu zinazopita miradi hiyo ya Bara bara sambamba na Ujenzi wa haraka wa madajara kutokana na hali bora ya hewa iliyopo hivi sasa wakati harakati za Ujenzi zikiendelea.

Kwa upande wao Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Hassan Khatib Hassan na yule ya Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud kwa niaba ya Wananchi wa Mikoa hiyo wameipongeza na kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa umakini wake wa kupambana na changamoto zinazowakabili Wananchi.

Wakuu hao wa Mikoa pamoja na mambo mengine kupitia Kamati zao za Ulinzi na Usalama katika hatua za awali wameshaweka mikakati ya kulitafutia ufumbuzi Tatizo la mwendo kasi katika Bara  bara tofauti ambapo Askari wa Usalama Bara barani watawekwa kuratibu Mwenendo wa matumizi wa Bara bara hizo.

Nao Wananchi wa Maeneo yaliyobahatika kupitishwa Bara bara hizo wameelezea kufarajika kwao na hatua ya Serikali kuona umuhimu mkubwa wa kuwapatia huduma hiyo ya Mawasiliano ya Bara bara.

 

 

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA WAMETAKIWA KUYAFNYIA KAZI KWA VITENDO MASOMO YAO

Serikali imeshauriwa kuwaajiri zaidi Vijana waliosoma katika Vyuo vya ndani ili kuongeza nguvu na hamasa kwa Wahadhiri wa Vyuo hivyo.

Akizindua Documentari iliyoandaliwa na Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza wa Chuo cha Utumishi wa Umma  (IPA) Makamu Mwenyekiti  wa Baraza la Chuo hicho Mh.Mohammed Said Dimwa Amesema kwa vile Vyuo vya Ndani vinasomesha Fani nyingi ni vyema Serikali ikawaajiri hadhi ya Vyuo vya Ndani.

Mrajisi wa Chuo hicho Nd. Mshauri Abdullah Khamis amewataka Wanafunzi hao kuyafanyia kazi kwa vitendo Masomo waliyopatiwa ili wafanikiwe malengo yao.

Wanafunzi wa Chuo hicho wameuomba Uongozi wa Chuo hicho kuongeza Majengo ili waweze kudahili Wanafunzi wengi hali itakayokiongezea hadhi zaidi Chuo hicho.

 

error: Content is protected !!