Viongozi wa Dini wametakiwa kukemea Rushwa na kutetea Watu wanyonge ili kazi yao izidi kuwa mfano bora kwa Jamii na kwa Taifa .
Hayo yameelezwa na Baba Askofu Augostino Shao katika ibada maalumu ya kumuweka katika daraja la Upatri Noberty Athanas Chilala kuwa Padri wa Parokia ya Kiboje jimbo la katoliki Zanzibar
Askofu Shao amemtaka Askofu Noberty kuwa mfano bora kwa vijana hasa katika kutumia ubunifu wake tatika kuwasaidia kuwapatia elimu ili waweze kujiajiri wenyewe .
Hata hivyo Askofu Shayo amewataka waumini hao kumpa ushirikiano ili kazi yake izidi kutukuka
Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika ibada hiyo wamesema kazi hii ni kazi ngumu na sio kazi rahisi inahitaji moyo hivyo kupatikana kwa padri huyo itawasaidia katika kuendeleza kazi ya kiroho katika Kanisa na kwa Taifa .
Nao Waumini wamefurahishwa kwa kumpata Padri Noberty na wamesema watazidi kumuombea na kumpa mashirikiano zaid.