Monthly Archives: August 2020

WASANII WA TASNIA YA FILAMU ZANZIBAR WAMEHIMIZWA KUWA NA TAALUMA YA UPIGAJI PICHA KATIKA FILAMU ZAO

Wasanii wa Tasnia ya Filamu Zanzibar, Wamehimizwa kuwa na Taaluma ya Upigaji Picha kwenye Filamu zao kwa madhumuni ya kuzalisha Filamu zenye ubora.

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ambae pia ni Mkufunzi  wa Mafunzo yanayondelea hapa ZBC, amewambia Wasanii kwamba katika kuzalisha Filamu zenye kiwango ni vyema kwa msimamizi Mkuu wa Filamu akaandaa mwenendo mzima wa kazi kimaandishi, huku wakizingatia suala la mashirikiano kwa wenye mamlaka katika maeneo wanayokwenda kurekodi Filamu zao.

Katika maoni yao Wasanii hao wamesema hali ngumu ya fedha inachangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha Filamu zisizo fikia viwango vya Kimataifa.

Mafunzo hayo ya siku 10 yameandaliwa na Ofisi ya haki Miliki Zanzibar kwa malengo ya kuwaongezea uwezo waandaaji wa Filamu Zanzibar.

 

 

KUPUNGUWA KWA TALAKA NI MAFANIKIO YA MAFUNZO YANAYOTOLEWA KWA JAMII NA WANANDOA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Khamis Juma Mwalimu amesema kupunguwa kwa Talaka ni mafanikio ya Mafunzo yanayotolewa kwa Jamii na Wanandoa kuwataka kuendelea na kuvumiliana ili mafanikio yazidi kuendelea.

Amesema Elimu ni jambo linasaidia kufikia malengo ya kila taifa ambalo linahitaji kuendelea na yaliyoendelea Kiuchumi.

Mhe, Khamis amesema hayo wakati akifunga mkupuo wa sita wa Mafunzo ya Ndoa kwa Wanafunzi 60 Waliohitimu mafunzo yanayoendeshwa na Ofisi ya Mufti.

Amesema katika Ndoa kuna mambo mengi ambayo yanahitaji kuvumiliana ili kuzitunza Ndoa zao na kulendelea kuzikataa Talaka ambazo sio nzuri.

Katibu wa Mufti Shehe Khalid Ali Mfaume amesema tokea kuanza kutolewa mafunzo ya Ndoa yapo mafanikio na talaka zimeanza kupunguwa na sasa Ndoa zinaanza kudumu.

Awali Wahitimu wa Mafunzo wameiomba Serikali kuongeza nguvu na kuweka Sheria ya kuwepo Stakabadhi Maalum kabla ya mtu kufunga Ndoa.

 

 

 

 

 

 

 

TIMU YA JKU ACADEMY IMEIFUNGA TIMU YA TAVETA CITY MABAO 5-2 KWENYE MASHINDANO YA YAMLE YAMLE

Timu ya JKU Academy imefanikiwa kupata alama tatu baada ya kuifunga timu ya TAVETA City mabao 5-2 kwenye mashindano ya Yamle Yamle mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Magirisi.

Vijana wa JKU Academy waliovalia Jezi Rangi nyekundu walionekanwa kuutawala Mchezo huo na kufanikiwa kupata mabao hayo 5 yaliyofungwa na Ahmed Khamis dk 36, Ramadhan Manzil dk 40, Mudrid Shehe dk 75 na Abubakar Hassan dk 50 na 80 huku mabao 2 ya Taveta cCty yakifungwa na Ali Haji dk 24 na Abrahman Juma dk 55.

Nahodha wa JKU Academy Abubakar Hassan amezungumzia siri ya ushindi wao.

Kwa upande wake Nahodha wa Taveta Mohd Iddi Duchi amesema walizidiwa na vijana wa JKU kutokana na kuwa pamoja muda mwingi kuliko wao wanaojuwana Uwanjani tu.

 

DKT MAGUFULI AMEAHIDI KUJENGA UWANJA MKUBWA WA KISASA WA MICHEZO DODOMA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa kisasa wa Michezo utakaokwenda sambamba na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.

Akizungumza katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma amesema hatua hiyo na nyenginezo zinalenga kuimarisha zaidi Jiji la Dodoma.

Dkt Magufuli amesema Watanzania wanataka mabadiliko katika Sekta mbali mbali jambo ambalo linatekelezwa katika hatua tofati.

Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kulinda Rasilimali za Madini, kupambana na Rushwa Ununuzi wa Ndege Mpya 11 na kurejesha nidhamu kwa watendaji wa Umma.

Aidha ameahidi kujenga Uwanja Mkubwa wa Ndege Mjini Dodoma utakaokuwa na uwezo wa kusafirisha Abiria moja kwa moja kuelekea Nchi za Nje.

Sambamba na hayo amesema Serikali itanunua Ndege nyengine mpya Tano ikiwemo ya kubebea Mizigo.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ali akitoa muhutasari wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 amesema inalenga kuhimiza Wananchi kuwa Wazalendo kwa Nchi yao na kutunza Rasilimali za Taifa ziwe chachu ya Maendeleo.

Amesema ataendelea kuilinda Amani na Mapinduzi ya Zanzibar ili kuimarisha maendeleo ya Tanzania.

error: Content is protected !!