Daily Archives: July 11, 2020

DK.SHEIN AMETOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA BALOZI MSTAAFU JOB LUSINDE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa Mkono wa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu Balozi Mstaafu job Malecela Lusinde aliyefariki Dunia Jumanne Julai 7, Mwaka huu.

Rais Dk. Shein alifika nyumbani kwa marehemu Balozi Mstaafu Job Lusinde majira ya asubuhi huko katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma mbapo alitoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki ikiwani pamoja na kumpampole Mjane wa Marehemu Sara Lusinde.

Akitoa mkono wake wa pole Rais Dk. Shein alieleza jinsi alivyoguswa na kifo cha aliyekuwa miongoni mwa Mawaziri 11 wa Kwanza wa Tanganyika ambapo alieleza kuwa kiongozi huyo Mkongwe wa siasa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na kiongozi wa Wazee wa Dodoma.

Aidha, Rais Dk. Shein alipata fursa ya kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Lusinde na kutoa heshima ya mwisho akiwa pamoja na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi mbali mbali hapo nyumbani kwake mtaa wa Uzunguni Mjini Dodoma.

 

Mapema Rais Dk. Shein alipofika nyumbani kwa Marehemu alitia saini kitabu cha maombolezi ambapo alitoa pole kwa kifo cha Mzee Balozi Job Lusinde kwa wafiwa wote, ndugu na jamaa huku akimuomba  Mwenyezi Mungu awape subira na aiweke roho ya Marehemu pahala pema.

 

Akitoa neno la shukurani kwa Rais Dk. Shein Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela alimshukuru na kumpongeza Rais Dk. Shein kwa kushiriki kikamilifu katika msiba huo na hatimae kuuaga mwili wa marehemu.

Mwanasiasa huyo mkongwe, Balozi Job Lusinde (90) alikuwa mmoja wa viongozi katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

 

Familia ya Balozi Lusinde na Malecela ilieleza kuwa taratibu za mazishi zinaendelea asubuhi hii na baadae mwili wa marehemu utapelekwa Kanisani kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyengine za mazishi. Marehemu Lusinde ni kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, John Samweli Malecela.

Marehemu Balozi Lusinde amezaliwa Oktoba 9, 1930 na aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961.

Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984 pamoja na kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Aidha, Marehemu Balozi Lusinde ndio kiongozi pekee aliyekuwa amebaki hai akiwa miongoni mwa Mawaziri wa Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwili wa kiongozi huyo unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kikuyu jirani na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana Jijini Dodoma.

Mara baada ya kutoa mkono wa pole Rais Dk. Shein ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alielekea katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

 

 

 

DK. HUSSEIN MWINYI ACHAGULIWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR

Chama cha Mapinduzi kimemchagua  Dr .Hussein Mwinyi kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM  katika  Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu. 

Drt hussein  atakuwa Mgombea wa kiti  hicho baada ya kuwashinda Wagombea wenzake walioingia katika nafasi  ya Tatu  bora kwa kupata kura 129 sawa na asilimia 78 .68  ambao ni Waziri Kiongozi Mstaafu Nd. Shamsi  Vuai Nahodha aliepata kura 16 na Dr. Khalid Salim Mohammed na  Mwakilishi wa Jimbo la Donge  aliepata kura  19. 

Dr .Hussen  Mwinyi  atapeperusha  Bendera  ya  CCM katika  kinyanganyiro  cha  kuwania  kurithi  Nafasi  ya  Urais  wa  Zanzibar  inayoachwa  na  Dr .Ali  Mohamed  Shein  anaemaliza  muda  wake  wa Uongozi  Mwishoni  mwa  Mwaka  huu 

Mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Kesho Jijini Dodoma baada ya Wajumbe wote wa Halmashauri kuu  Taifa kumpitisha bila ya kupingwa  Mwenyekiti   wa  Chama  hicho  na Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Dr .John  Joseph  Pombe  Magufuli.                                                 

 

WANANCHI ZANZIBAR WAKIPONGEZA CCM KWA KUMTEUA DK. HUSSEIN MWINYI KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR

 Wananchi wamekipongeza Chama cha Mapinduzi kwa Kumchagua Dr. Hussein  Ali Mwinyi kuwa  Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya  Chama  hicho  katika  Uchaguzi Mkuu Ujao. 

Wakizungumza  na  ZBC   katika Maeneo Tofauti  wamesema  Dr. Hussein ni  mweledi  na  anaifahamu vyema  Zanzibar na  Wanatarajia kuwa  ataweza kukidhi kiu ya Wananchi  hasa kwa kuendeleza pale atakapomalizia  Dkt .Shein. 

Dkt. Hussein  ambae sasa  ni  Waziri  wa  Ulinzi  wa  Serikali  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania wakati akijieleza  mbelea  ya Mkutano  Jijini  Dodoma ameahidi  kuyalinda  na Mapinduzi  ya  Zanzibar  na  Muungano  wa  Tanzania. 

 

 

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA KIJANGWANI WAMEIOMBA SERIKALI KUWAIMARISHIA MIUNDO MBINU YA SOKO HILO

 

Wafanyabiashara wa Soko la Kijangwani wameiomba Baraza la Manispaa ya Mjini kuimarisha Miundombinu ya katika Soko hilo iwapo litaamuliwa kuwa la kudumu. 

Wakizungumza na Camera yaBiashara ZBC  wamesema mazingira  ya  Biashara bado  sio  mazuri  iukilinganisha  na  Masoko  wanayotoka  ya Mwanakwerekwe, Darajani  na  Mombasa  Shimoni  kutokana  na  kuwa  na  idadi  ndogo  ya Wateja. 

Changamoto  nyengine  walioielezea  ni  kukosekana  kwa  Eneo  muafaka  la  kuhifadhia  bidhaa  zao  hasa  wakati  wa  Mvua  na  kuomba   Baraza  la  Manispaa  ya  Mjini  kulipatia ufumbuzi  tatizo  hilo. 

Afisa Uhusiano wa  Manispaa  ya Mjini  Nd.Seif  Ali  Seif  amewashauri  Wafanyabiashara hao kuwa   wastahimilivu  kwani  kituo hicho ni cha muda na siyo cha kudumu kwa shughuli ya Biashara. 

Wakati  huohuo  ZBC  imetembelea Soko la   Ijitimai  na  kukuta Soko hilo  likiwa  tupu  bila  ya  Wafanya Biashara  bila  ya  kujuwa  sababu  ya   hali  .