Daily Archives: July 10, 2020

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI UMEKAMILIKA JIJINI DODOMA

Maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi utakaothibisha mgombea wa Urais Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama  hicho yamekamilika . 

ZBC imeshuhudia baadhi ya wagombea wa urais wa Zanzibar kupitia CCM wakiwasili Makao Makuu ya CCM Dodoma tayari kushiriki kikao hicho .

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kinatarajiwa kufanyika kesho kuchagua jina moja la mwanachama atakaesimama kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi ujao  

Mkutano mkuu wa  CCM  unatarajiwa  kufanyika Jumamosi hii ambapo pamoja na mambo mengine utathibisha jina la Mgombea wa nafasi ya Urais kuwasilisha ripoti za utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi