Daily Archives: June 11, 2020

JUMUIYA YA MUZDALIFA IMEISAIDIA WIZARA YA ELIMU PRINTA 130

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma Amesema si busara kwa Walimu kuvujisha mitihani kwa Wanafunzi kwani vitendo hivyo vinashusha hadhi ya Elimu Nchini.

Amesema katika kudhibiti hali hiyo wanapaswa kuendelea kushirikiana na Walimu Wakuu ili kusimamia pamoja na kuweka mikakati bora ya kuondosha vitendo hivyo ikiwemo ufuatiliaji wa Masomo kwa Wanafunzi.

Akizungumza baada kupokea msaada wa Printa 130 kutoka Jumuiya ya Muzdalfa, Mhe. Riziki ameishukuru Taasisi hiyo  kwa kusaidia ukuaji wa Sekta ya Elimu Zanzibar na kusema hatua hiyo italeta mageuzi katika utendaji wa kazi za Skuli.

Mwenyekiti  wa Muzdalifa Nd. Abdalla Hadhar Abdalla amesema wametoa vifaa hivyo kuondosha matatizo yanayozikabili Skuli mbali mbali ya kutumia Ofisi za Nje kwa kazi zao kitendo ambacho kinasababisha kuvuja kwa baadhi ya siri ikiwemo mitihani.

Zaidi ya Shillingi Millioni 34 zimetumika kwa ununuzi wa Vifaa hivyo.

SEKTA YA UTALII NCHINI IMEJIPANGA KUIMAIRISHA HUDUMA BORA ZA KINGA YA MARADHI YA CORONA

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mh.Mahmoud  Thabit Kombo amesema Serikali imejipanga kuweka huduma bora za kinga za Maradhi ya Corona katika Maeneo mbali mbali wanayofikia Wageni Nchini.

Akizungumza katika Mkutano maalum na Wadau wa Sekta ya Utalii kujadiliana kuhusu mandalizi ya kuwapatia huduma muhimu za Afya ili kujikinga na Corona ikwemo Uwanja wa Ndege  na Hoteli mbali mbali Nchini.

Katibu Mtendaji wa  Kamisheni ya Utalii Dk .Abdalah  Muhammed Juma amesema  miongozo iliyoainzishwa kwa ushirikiano na Wadau  wa Sekta hiyo itasaidia kuendesha Biashara ya Utalii italeta tija kwa Serikali na Wananchi wake.

Baadhi ya Wadau hao walioshiriki Mkutano huo wamesema  bado tahadhari kubwa zinahitaji kuchukuliwa kwa Wageni na Wananchi kuendelea  kuwa salama na Maradhi ya Corona ili kuweza kuimarisha utendaji wa Sekta hiyo ya Utalii Zanzibar

 

KIWANJA CHA URITHI CHA SABABISHA MGOGORO

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Magharibi “b” Captain Silima Haji amesitisha Ujenzi wa Nyumba unaondelea katika Eneo linalodaiwa kuwa na mgogoro wa Ardhi liliopo Shehia ya Kipungani.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Magharibi “b’ Captain Silima Haji ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya pande mbili baina ya Familia ya Omar Hassan Fatih na Familia ya Salma Mussa Machano ambapo kumejitokeza baadhi ya Wanafamilia kuuza Shamba hilo bila maelewano.

Captain Silima amesema kutokana na kutokuwepo kwa Mmiliki halali wa Shamba hilo serikali ya Wilaya imeamua  kusitisha Ujenzi huo hadi utakapopatikana ushahidi  wa Mmliki halali wa Shamba hilo.

Msemaji wa Familia ya Bwana Omar Salum Fatih Amesema Eneo hilo ni mali ya urithi ambao umeachiwa Familia kutokana na kuwa Mmiliki wa Eneo hilo hakuwa na Mtoto.

Nae Bi.Salma  Mussa Machano ambae ni Mlalamikaji wa Shamba hilo amesema kutokana na Mgogoro  uliobuka  tayari wameshapeleka sehemu husika  na kuiomba Serikali kulipatia ufumbuzi  unaofaa.

 

 

error: Content is protected !!