Daily Archives: June 10, 2020

UJENZI WA ENEO LA MAEGEGESHO YA NDEGE WA ZANZIBAR ZIMEANZA BAADA YA KUSITA KWA MUDA MREFU

Kazi ya Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Eneo la Maegegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar  Terminal Three zimeanza baada ya kusita kwa muda mrefu.

Ujenzi huo unaendelea zuri katika sehemu za kupakia na kushukia Abiria ambapo Wahandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJ kutoka China wakishirikiana na Wahandisi Wazalendo kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Serikali Iddi alishuhudia harakati hizo pale alipofanya ziara maalum ya kukagua Maendeleo ya radi huo utakaokuwa wa Kihistoria wakati Zanzibar inakusudia kurejea katika hadhi yake ya kuwa kituo cha biashara Duaniani katika ukanda wa mashariki na kusini mwa Bara la Afrika.

Meneja wa Ujenzi wa mradi huo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Yasir De Costa alisema kazi ya Ujenzi wa Mradi huo hivi sasa imeshafikia asilimia 71% na ile asilimia 29% iliobakia inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi michache ijao.

Mhandisi De Costa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Meli iliyobeba zana na vifaa vya kuendeleza mradi huo kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China hivi sasa imeshawasili katika Bandari ya Zanzibar na utaratibu wa kuvishusha ili vifikishwe katika eneo husika unakamilishwa.

Alisema Wahandisi wa Mradi huo wamejipangia kumwaga zege urefu wa Mita Hamsini (50) kwa siku kazi inayokwenda sambamba na ujenzi  wa miundombinu ya misingi ya kupitishia maji machafu pamoja na mikonge ya kupitishia Abiria .

Alibainisha kwamba ubadilishaji wa maegesho yatakuwa upande wa Kusini wa jengo la Abiria badala ya ile ya mbele kwa mfumo uliokubalika awali mabadiliko yaliyofanywa kuzingatia ushauri wa Wataalamu waliobobea ambao enbeo la mbele litaendelea kutoa huduma za kupita Ndege.

Mhandisi De Costa alifafanua kwamba kutokana na kasi kubwa za Ujenzi huo kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa Ndege ya kwanza inaweza kutua na kupata huduma katika eneo hilo jipya ifikapo mwezi oktoba mwaka huu.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili  wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi pamoja na wale wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa Ujenzi huo licha ya kuchelewa lakini kazi inaendelea vizuri na kutia moyo ili ile kiu ya Wananchi ifikie kikomo.

Balozi Seif alisema Uwanja wa Ndege wa Zanzibar umepata msukosuko wa mtaji wa Fedha wa kuendesha Mradi huo hadi pale Viongozi Wakuu walipofikia ufumbuzi kutokana na umakini  waliouonyesha kuhakikisha kwamba mradi huo unakamilika kama ilivyopangwa.

Alielezea faraja yake kutokana na uzalendo wa timu ya Wahandisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu juluis Kambarage Nyerere ikiongozwa na Mhandisi Mahiri na Jabari Rehema Myeya kusaidia ushauri wa kitaalamu katika maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliutaka Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya kuhudumia idadi kubwa ya abiria wanaoshuka na kuondoka pale matengenezo ya mradi huo yatakapokamilika.

error: Content is protected !!