Daily Archives: June 7, 2020

ZANZIBA YAFUNGUA SAFARI ZA UTALII

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuruhusu tena Ndege za Kitalii na za Biashara zikiwemo za moja kwa moja (Charter flights) kuanza rasmi Safari zake hapa Zanzibar kuanzia leo tarehe 06 juni, 2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari na baadhi ya Watendaji wa Serikali Waziri wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale hiyo     Mh. Mahmoud Thabit Kombo amesema hatua hiyo imefuatiwa baada ya Serikali kupitia Wizara hiyo kutangaza kusitisha rasmi Safari za Kitalii na Biashara mnamo tarehe 23 Machi, 2020 kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa Maradhi ya Corona.

Mh. Mahmoud amezitaka Taasisi zinazohusika na Utalii kuandaa Mazingira mazuri yatakayowezesha kupokea Watalii hao wakati wowote kuanzia leo pamoja na kuzingatia Masharti yote ya Afya na mengine ambayo yamewekwa kwa ajili ya kuendesha shughuli hizo.

Amesema Serikali pia itaweka utaratibu Maalum wa kudhibiti Watu wasiokuwa na Shughuli maalum kuingia katika Maeneo ya Utalii na kuzurura ovyo katika Fukwe na Eneo la Mji Mkongwe.

Aidha  amefahamisha kuwa  Serikali pia inakusudia kuweka mkazo katika kuimarisha Utalii wa Ndani na wa Masafa mafupi kwa kutumia Soko la Afrika na Nchi za Kiarabu ili kuhakikisha Nchi yetu inanufaika na Utalii wa Kimataifa kwa haraka zaidi.

WAZIRI AKABIDHI VIHORI 250 KWA WAKULIMA WA MWANI WA MKOA WA KUSINI UNGUJA

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imekabidhi Vihori vya kuchukulia Mwani kwa Kamati za Uvuvi za Shehia za Mkoa wa Kusini Unguja.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri Amesema Vihori  hivyo vitarahisisha kazi ya Ubebaji wa Mwani kutoka kina Kirefu cha Maji

Amesema kutokana na Mazingira magumu ya Ukulima wa Mwani Serikali inafanya mbinu mbali mbali za kuongeza thamani ya Kilimo hicho katika Soko la Dunia na Wakulima kupata Maslahi bora.

Baadhi ya Wakulima wa Mwani wamesema hatua hiyo ni Ukombozi katika kuendeleza Kilimo hicho kinachosaidia kukuza Uchumi wao itakayoendana na lengo la Serikali la kujenga Kiwanda cha kusarifu zao la Mwani Nchini.

Jumla ya Vihori 250 vyenye Thamani ya Shilingi Milioni Mia mbili vimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia kupitia mradi wa Swiofish.

LIGI KUU ZANZIBAR KUENDELEA KITUO KIMOJA UNGUJA

Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Nd. Hassan Omar King, Amesema ligi kuu Zanzibar, itachezwa katika Kituo kimoja cha Unguja ili kupunguza gharama nyingine za uendeshaji.

Amesema Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo la kujikinga na Virusi vya Corona.

ELFU SABA YASABABISHA MTOTO KUCHOMWA MIKONO MOTO

Mtoto Mmoja mkaazi wa fukuchani  amechomwa moto Mikono kwa madai y a kuiba elfu saba.

Akimtembelea Mtoto huyo katika Hospital ya Kivunge kwa lengo la  kumpa pole  Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini a Unguja  Nd. Hassan Ali Kombo akifuatana na kamati ya Ulinzi na Usalama amesema kuwa atashirikiana na Ustawi wa Jamii kuhakikisha mtuhumiwa huyo anafikishwa katika Vyombo vinavyohusika kwa kuchukuliwa hatua.

Nae  Mtoto  Shafii  Ali  Mwenye Umri wa Miaka 13 anaesoma Skuli ya Fukuchani alieleza jinsi tukio lilivotokea aliseme alikua anatoka kulala kwa Babu yake akachukua Chakula kuwapa Kuku ndio akaitwa na Mama yake mdogo na kumfunga kamba baadae akamwaga mafuta kwenye mikono na kumchoma moto.

Kwa niaba ya Madaktar  Dokta Ame Mngwali Khamis ameishukuru Ofisi ya  Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini a Unguja kwa kuwa karibu sana na Hospitali hiyo  Amesema na kuwaomba Wananchi waache kujichukulia sheria Mikononi mwao ili kuondosha vitendo kama hivyo vya Uzalilishaji.

Kwa niaba ya Ofisi ya Ustawi wa Jamii Afisa wa Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndugu  Khamis Kona Khamis amesema watahakikisha Ofisi yake italifuatilia suala hilo mpaka kuona haki inatendeka

error: Content is protected !!