Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Mh: Abdallah Ulega Amesema Uzalishaji wa Mazao ya Bahari unahitaji kufanyiwa Mabadiliko makubwa kwa kuwa ndio Nguzo Kuu ya kukuza kipato kwa Wakaazi wa Ukanda wa Bahari ya Tanzania.
Amefahamisha kuwa licha ya Tanzania kuelekea Mpango wa Uvuvi wa Bahari Kuu ipo Miradi midogo ukiwemo wa Ufugaji wa Samaki na Majongoo inanafasi ya kuleta Mageuzi makubwa ya Kiuchumi katika Ukanda huo
Akizungumza katika Kituo cha utotoaji wa Vifaranga vya Samaki, Majongoo na Kaa huko Maruhubi katika Ziara Maalum Zanzibar Mh.Ulega Amesema Mabadiliko hayo yataendana na mikakati ya Serikali zote Mbili za Tanzania za kufanya Mapinduzi kwa Sekta ya Uvuvi ili kukuza Maendeleo kwa haraka.
Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili na Mifugo, Dk.Makame Ali Ussi, ameeleza kuwa Zanzibar inaendelea na mpango wa Uchumi wa Bahari, kwa kuwa unanafasi kubwa ya kuingiza Mapato ya haraka pamoja na kuwanufaika Wananchi wengi
Katika Ziara hiyo Mh.Ulega ametambelea pia Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Baharini ambapo kwa Pamoja alipata maelezo kutoka kwa Watendaji wa Taasisi hizo.