Daily Archives: June 2, 2020

WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WAMEANZA RATIBA ZAO ZA MASOMO BAADA YA KUPUNGUA UGONJWA WA CORONA

Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu wakiwamo wa Vyuo na Kidato cha Sita wameanza Ratiba zao za Masomo baada ya kufunguliwa kufuatia kupungua Ugonjwa wa Corona.

Jijini Dar-es-salaam, ZBC imetembelea Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM na kujionea harakati za Wanachuo  zikiendelea kwa kuwa katika hali ya Tahadhali.

Nae Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanachuo cha IFM nd. Derick Steven Mallya  anaelezea  juu ya Taratibu za Taaluma  sambamba na Mazingira ya tahadhali ya Ugonjwa wa Korona.

Nao Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Tambaza iliyoko Manispaa ya Ilala wameanza Masomo yao  kwa mwongozo wa Wataalamu wa Afya  juu ya namna ya kukaa kwa kuzingatia umbali tofauti na ilivyokuwa zamani.

error: Content is protected !!