Daily Archives: June 1, 2020

UHARIBIFU WA VIPANDO WAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MATEMWE

  Wakaazi wa Kijiji cha Matemwe wameiomba Serekali kufuatilia uharibifu wa Vipando vyao unaodaiwa kufanywa na Muekezaji katika Maeneo wanayoyatumia kwa Kilimo.

Wakizungumza na ZBC Wakaazi hao wameelezea kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Muwekezaji huyo kwani hawakupewa taarifa yeyote juu ya Eneo hilo kuwa amepewa Muwekezaji.

Wamesema Ardhi ni mali ya Serekali hivyo wameziomba Mamlaka husika kulifuatilia suala la kuharibiwa Vipando vyao kwani ndio shughuli zao za kuendesha Maisha.

Akizungumza na Wakaazi hao Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Maliasili na Uvuvi Dk. Makame Ali Ussi amesema ameyapokea malalamiko hayo na atayafikisha sehemu husika ili yafanyiwe kazi na amewataka Wakaazi hao kuondoa hofu kwa vile suala hilo tayari limefika Serikalini.

error: Content is protected !!