Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Serikali itaendelea kuliunga mkono Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutekeleza Majukumu ya Kitafa ikiwemo Ujenzi na Uzalishaji Mali.
Mhe. Rais Magufuli ameeleza kuwa Serikali imeamua kutekeleza Azimio la kuhamia Dodoma ambapo tayari Wizara zote, Watumishi, Viongozi Wakuu akiwemo yeye Mwenyewe tayari ameshahamia na Jeshi hilo limefanya kazi kubwa kufanikisha Ujenzi huo.
Akizungumza katika Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi Kuu za Ikulu Dodoma ameipongeza Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) ambayo ni Mkandarasi Mshauri wa Mradi huo na kumuagiza Waziri wa Fedha Dkt. Philip mpango kutoa shilingi Bilioni 2 ili Jeshi hilo likamilishe Ujenzi huo kwa muda wa miezi 5 walioahidi.
Rais Pombe Magufuli, ameweka jiwe hilo la msingi kwa kushirkiana na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Majengo 6 ya Ofisi za Ikulu Dodom yanajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika eneo la Vikonje Jijini Dodoma yanayotarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 5 ijayo ambapo tayari baadhi ya majengo mengine ikiwemo Nyumba ya Makazi ya Rais, Ofisi mbalimbali na ukuta wenye urefu wa kilometa 27 yamekamilika.