Daily Archives: April 6, 2020

KAZI YA UWEKAJI WA TAA ZA BARABARANI KISIWANI PEMBA INAENDELEA

Kazi ya Uwekaji wataa za  Barabarani  Kisiwani  Pemba inaendelea vizuri licha ya Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha

Akizungumza mara baada ya kumaliza Ziara ya kuangalia kazi inavyo endelea kwa kasi katika Miji ya Wete Mkoani na kisha kuona majiribio ya Taa hizo zikiwashwa katika eneo la MachoManne Chake Chake

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usaju  ambayo imepewa kazi ya uwekaji Taa hizo Nd.Ussi  Salum  Pondeza amesema Kampuni ina tarajia kutumia zaid ya sh Bilioni 6.2  inakwenda kama walivyo iyahidi Serekali

Akizungumza na Waandishi wa Habari huko MachoManne Chake Chake juu ya maendeleo ya kazi hio   msimamizi Mkuu wa Taa za Barabarani Zanzibar Injinia Fadhili Omar Kilala amesema kazi hio ya uwekaji Taa Barabarani  kwa Wilaya ya Chake Chake umeshafikia Asilimia 75 na mara baada ya kumaliza Chake Chake na Mkoani  wataelekea  kumalizia Wete kazi ya Uwekaji Taa za Barabarani

Kisiwani Pemba kumeanza kung`arisha baadhi ya maeneo ya Kisiwa hicho baada ya Taa kuanza kuwaka Wananchi wakisifia kuondokana na adha Vibaka kuwapora na kuwapiga bodi nyakati za usiku kwenye Madirisha ya Nyumba zao wakiwa Wamelala

error: Content is protected !!