Daily Archives: April 5, 2020

SHUGHULI ZA UANIKAJI DAGAA ZASIMAMISHWA ILI KUNUSURU MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi imesimamisha shughuli za uanikaji Dagaa katika Kambi ya Shehia ya kihinani ili kunusuru maambukizi ya Virusi vya CORONA.

Akizungumza na Wafanyabiashara wa Mkaa, wavuvi na waanika Dagaa wa Kihinani.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Nd. Hassan Khatib amesema uamuzi huo wa kuondosha mikusanyiko ya Watu una lengo la kunusuru maambukizi ya Virusi vya CORONA hivyo amewataka Wananchi  kuwa wastahamilivu na kufuata maelekezo ya Serikali na ya Wataalamu wa Afya.

Mkurugenzi Manispaa ya Magharibi "A" Nd. Amour Ali Mussa amesema Uongozi wa Manispaa hiyo utaendelea kushirikiana na Viongozi wa Jumuiya za Wafanya Biashara wa maeneo hayo ili Elimu ya afya iendelee kutolewa kuepusha kuenea kwa Ugonjwa wa CORONA.

WAJASIRAMALI KUJENGEWA UWEZO WA UZALISHAJI WA BIDHAA

 Serikali ya Mapinduzi ya zzanzibar imepanga mikakati maalum ya  kuwainua wajasiramali kwa kuwajengea uwezo wa uzalishaji wa bidhaa zilizobora ili ziweze kuuzika ndani na nje ya Nchi

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko amesema Wizara yake  imeamua kutwaunga mkono Wajasiriamali wa hapa Zanzibar kwa kuwatafutia Soko bidhaa zao sambamba na kuwajengea Viwanda ambavyo vitawasaidia katika uzalishaji wa  Bidhaa zao

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala Maendeleo ya Viwanda vidogovidogo SMIDA amesema kwa sasa wameamua kutoa Mafunzo kwa Wajasiria mali juu ya utengenezaji wa vitakasa mikono (sanitizer) kwakuwa bidhaa hiyo kwa sasa imekuwa ikihitaajika kwa wingi

Afisa wa Wakala wa Dawa na Vipodozi ZFDA amesema bidhaa ambazo zitatengezeza na Wajasiriaa mali hao zitakuwa zimefuata vigezo vyote ambazo vinatakiwa kuwemo ndani ya bidhaa hizo kwa maelekeze ya Shirika la Afya Duniani WHO

Wajasiria mali hao wameahidi kuyatumia vyema mafunzo hayo na wamewataka Wananchi kuacha tabia ya kutengeneza bidhaa hizo bila ya kufuata utaratibu kwa lengo la kujipatia kipato

error: Content is protected !!